Akidi ya Wazee
Majukumu


Picha
kikundi cha wanaume wakiwa wamekaa pamoja

Wito wangu kama Mshauri katika Urais wa Akidi ya Wazee

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Akidi ya Wazee

Ukuhani wa Melkizedeki unawasaidia watoto wa Mungu kujiandaa kurudi katika uwepo Wake. Washiriki wa akidi ya wazee hufanya kazi pamoja ili kusaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Wanawahudumia wengine, wanatimiza wajibu wa ukuhani, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 8.1).

Washauri

Washauri katika akidi ya wazee wanamsaidia rais katika majukumu yake ya kupanga jitihada pamoja na urais wa Muungano wa Usaidizi na kusimamia utumishi, shughuli, ripoti, kumbukumbu na fedha. Washauri kutoka akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanaweza kupangiwa kuongoza kazi ya umisionari katika kata au jitihada za kazi ya hekalu na historia ya familia (ona 8.3.3.2).

Urais

Urais wa akidi ya wazee na katibu hukutana mara kwa mara. Kuwasaidia wazee watarajiwa kujiandaa kupokea Ukuhani wa Melkizedeki ni moja ya vipaumbele vya juu zaidi vya urais wa akidi (ona 8.4).

Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi

Urais wa Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi huratibu majukumu ya kuhudumu na kusaidia kuongoza kazi ya hekaluni na historia ya familia na juhudi za kuwaalika wote kupokea baraka za injili. Pia wana jukumu muhimu katika kuwafundisha waumini katika kata kanuni za kuhudumia, mahojiano ya kuhudumia, kuishi sheria ya mfungo, kukuza kujitegemea, na kuongeza utayari binafsi na wa familia (ona 22.6.2).

Mikutano ya Jumapili

Akidi ya Wazee hukutana Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi ili kuongeza imani, kujenga umoja, na kuimarisha familia na nyumba. Urais wa akidi ya wazee kwa sala huchagua jumbe kutoka kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni zaidi ili kujadili kulingana na mahitaji ya washiriki (ona 8.2.1.2).

Huduma na Shughuli

Urais wa akidi ya wazee wanaweza kupanga shughuli za kuwaimarisha washiriki wa akidi na kuwapa fursa za kutumikia pamoja. Urais unajadili shughili hizo pamoja na askofu (ona 8.2.1.3).

Chapisha