Wito wangu kama Mshauri wa Urais wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Muungano wa Usaidizi
Muungano wa Usaidizi ni kikundi kitakatifu kilichoanzishwa kwa ajili ya wanawake watu wazima wote katika Kanisa. Muugano wa Usaidizi unawasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba dhumuni la Muungano wa Usaidizi ni “kuokoa nafsi na kuondoa mateso”—kutoa faraja ya Mwokozi (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 9.1).
Mshauri wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi
Washiriki wa urais wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi wana majukumu mengi ambayo yanajumuisha kuwaelekeza urais mpya wa Muungano wa Usaidizi katika kata na kutoa msaada endelevu; kuwafundisha marais wa Muungano wa Usaidizi katika kata kanuni za kuhudumu, historia ya familia, na kazi ya umisionari (ona 9.5); kuwaimarisha akina dada waseja; kuratibu juhudi za dharura; kuzungumza katika mikutano ya sakramenti na mazingira mengine; na kutembelea mikutano ya Muungano wa Usaidizi katika kata (ona 6.7.1).
Mikutano na Mabaraza
Urais wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi hushauriana pamoja mara kwa mara. Mshiriki wa urais anahudumu kwenye kamati za kigingi za vijana wakubwa waseja na watu wazima waseja, ikiwa imepangwa. Urais unahudhuria mikutano ya uongozi ya kigingi kila mwaka na huwaelekeza urais wa Muungano wa Usaidizi katika kata kwenye mikutano hiyo (ona 29.3.4), unahudumu kwenye kamati ya uongozi ya kigingi ya watu wazima, na unahudhuria mikutano ya baraza la uratibu wakati wanapoalikwa na Sabini wa Eneo (ona 29.4).
Huduma na Shughuli
Urais wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi unaweza kupanga mkutano mmoja au miwili kila mwaka kwa ajili ya akina dada wote wa Muungano wa Usaidizi katika kigingi. Mikutano hii inaweza kujumuisha huduma, madarasa, miradi, mikutano, au warsha (ona 6.7.1.1). Urais wa Muungano wa Usaidizi katika kigingi, wa Wasichana, na wa Watoto mara kadha wa kadha wanaweza kupanga shughuli za pamoja kwa ajili ya vikundi vyao (ona 6.7.1).
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera vinapatikana katika sehemu ya 9.6 ya Kitabu cha Maelekezo ya Jumla.