Shule ya Jumapili
Majukumu


Picha
kundi la watu wakitabasamu

Wito wangu kama Mshauri katika Urais wa Shule ya Jumapili

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Kusudi la Shule ya Jumapili

Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Hufanya hivyo kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 13.1, Maktaba ya Injili).

Urais wa Shule ya Jumapili

Rais ana wajibu wa kuhudumu katika baraza la kata, kusimamia ufundishaji na kujifunza injili nyumbani na kanisani, na kuanzisha madarasa. Washauri wake humsaidia. Urais wa Shule ya Jumapili huunga mkono, huamasisha, na kuwaelekeza walimu kuwa na ufanisi zaidi kwa kufuata kanuni katika maandiko na Kufundisha katika Njia ya Mwokozi (ona 13.2.2.2).

Madarasa ya Jumapili

Madarasa ya Shule ya Jumapili hufanyika Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi. Ukubwa wa darasa hutofautiana kulingana na mahitaji ya kila kata (ona 13.3). Walimu wa Shule ya Jumapili hutumia maandiko, masomo yaliyopangwa ndani ya Njoo, Unifuate, na maneno ya manabii wa sasa kama nyenzo zao kuu za kufundishia.

Mafunzo Yanayolenga Nyumbani

Wazazi wanawajibika kuwafundisha injili watoto wao. (ona 13.5). Walimu wa Shule ya Jumapili na viongozi huwahimiza waumini kutafuta mwongozo wa kiungu wao wenyewe kuhusu jinsi gani ya kujifunza na kufundisha injili katika nyumba zao (ona 17.2).

Mikutano ya Baraza la Walimu

Washauri humsaidia rais wa Shule ya Jumapili kupanga na kuendesha mikutano ya baraza la walimu. Katika mikutano ya baraza la walimu, walimu hushauriana kwa pamoja kuhusu kanuni za ufundishaji kama wa Kristo. Pia hushauriana kuhusu jinsi ya kuboresha kujifunza injili na kuifundisha. Kufundisha katika njia ya Mwokozi hutumika kama nyenzo (ona 17.4). Mikutano hii hufanyika kila robo ya mwaka wakati wa darasa siku ya Jumapili na kwa kawaida huongozwa na rais wa Shule ya Jumapili (ona 13.4).

Mikutano ya Baraza la Walimu kwa ajili ya Wazazi

Washauri humsaidia rais wa Shule ya Jumapili kupanga na kuendesha mikutano ya baraza la walimu kwa ajili ya wazazi. Mkutano huu hufuata mpangilio sawa na ule wa mkutano wa baraza la walimu, isipokuwa wazazi hualikwa kuhudhuria. Kusudi ni kuwasaidia wazazi kuwa walimu bora katika nyumba zao. Kufundisha katika njia ya Mwokozi hutumika kama nyenzo (ona 17.4).

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo ya ziada ya Shule ya Jumapili hupatikana katika sehemu ya 13.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha