Akidi za Ukuhani wa Haruni
Majukumu


kundi la wavulana

Wito Wangu kama Mshauri katika Akidi ya Mashemasi

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Ukuhani wa Haruni

Akidi za ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho 10.1, Maktaba ya Injili.)

Akidi ya Mashemasi

Wavulana wanajiunga na akidi ya mashemasi katika Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 12. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa mashemasi kama wamejiandaa na wanastahili. Kazi zao ni pamoja na kupitisha sakramenti na kumsaidia askofu katika “kusimamia mambo yote ya kimwili” (Mafundisho na Maagano 107:68). (Ona 10.1.3.1.)

Mshauri

Washauri katika akidi ya mashemasi wanamsaidia rais katika majukumu yake, ikijumuisha kuongoza juhudi za akidi katika kushiriki kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa; kupata kumjua na kumhudumia kila mshiriki wa akidi, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mikutano ya akidi; kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi; kuwafundisha washiriki wa akidi kazi zao za ukuhani; na kupanga na kuendesha mikutano ya akidi (ona 10.4.2). Urais wa akidi unapaswa kukutana mara kwa mara (ona 10.4.3).

Huduma na Shughuli

Uaskofu na viongozi wa akidi ya vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Hizi zinapaswa kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Shughuli zinapaswa kuwa na usawa miongoni mwa maeneo manne ya ukuaji binafsi: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana, na kukusanya matoleo ya mfungo, zinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.