Wito Wangu kama Rais wa Akidi ya Mashemasi
Majukumu
Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Lengo la Ukuhani wa Haruni
Akidi za ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, Gospel Library.)
Akidi ya Mashemasi
Vijana wanaijunga na akidi ya mashemasi kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa mashemasi kama wamejiandaa na wanastahili. Kazi ni pamoja na kupitisha sakramenti na kumsaidia askofu katika “kusimamia mambo yote ya kimwili” (Mafundisho na Maagano 107:68). (Ona 10.1.3.1.)
Rais
Majukumu ya rais wa akidi ya mashemasi yanajumuisha kuongoza juhudi za akidi katika kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa; kupata kumjua na kumhudumia kila mshiriki wa akidi, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mikutano ya akidi; kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi; kuwafundisha washiriki wa akidi majukumu yao ya ukuhani; na kupanga na kuendesha mikutano ya akidi (ona 10.4.2). Washauri wake wanamuunga mkono katika majukumu yake. Urais wa akidi unapaswa kukutana mara kwa mara (ona 10.4.3).
Baraza la Vijana
Rais wa akidi ya mashemasi ni mshiriki wa baraza la vijana la kata. Lengo la baraza hili ni kuwasaidia vijana kuwaleta wengine kwa Yesu Kristo na kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Askofu anasimamia baraza la vijana la kata. (Ona 10.4:4.)
Huduma na Shughuli
Uaskofu na viongozi wa akidi ya vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Haya yanapaswa kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Mambo haya yanapaswa kuwa na usawa miongoni mwa maeneo manne ya ukuaji binafsi wa: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana, na kukusanya matoleo ya mfungo, vinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.