Akidi za Ukuhani wa Haruni
Majukumu


kundi la wavulana

Wito wangu kama Katibu katika Akidi ya Mashemasi

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Ukuhani wa Haruni

Akidi za ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, Maktaba ya Injili.)

Akidi ya Mashemasi

Vijana wanajiunga na akidi ya mashemasi kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 12. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa mashemasi kama wamejiandaa na wanastahili. Majukumu ni pamoja na kupitisha sakramenti na kumsaidia askofu katika “kusimamia mambo yote ya kimwili” (Mafundisho na Maagano 107:68). (Ona 10.1.3.1.)

Katibu

Wakati makatibu wa akidi wanapokuwa wameitwa, wao ndio wanaotayarisha ajenda kwa ajili ya mikutano na kuandika mihutasari ya mikutano hiyo. Pia wanamsaidia karani wa kata au mshauri wa akidi kuweka kumbukumbu za mahudhurio. (Ona 10.4:2.)

Huduma na Shughuli

Uaskofu na viongozi wa akidi ya vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Hizi zinapaswa kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Shughuli hizo zinapaswa kuwa na uwiano miongoni mwa maeneo manne ya ukuaji binafsi: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana, na kukusanya matoleo ya mfungo, zinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.