Msingi
Majukumu


kundi la wanawake na watoto

Wito Wangu kama Kiongozi wa Darasa la Awali

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Madhumuni ya Msingi

Msingi huwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha; kuishi injili ya Yesu Kristo; na kuhisi, kutambua na kutenda juu ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Msingi pia ni wakati wa kujiandaa, kufanya na kuweka maagano matakatifu pale watoto wanaposhiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)

Kiongozi wa Darasa la Awali

Kufundisha watoto wa Mungu ni fursa takatifu. Darasa la awali linawasaidia watoto wenye umri wa miezi 18 hadi miaka 3 wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha. Viongozi wa Darasa la Awali wanaupendo, wanafundisha, na kuwahudumia watoto. Pia wanahakikisha usalama na ustawi wao (ona 12.1.5).

Darasa ya Jumapili

Viongozi wa Darasa la Awali hufundisha kutoka Behold Your Little Ones. Wanafuata kanuni katika Kufundisha katika Njia ya Mwokozi na sura ya 17 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla. Wakati watu wazima wanapowafundisha watoto katika mipangilo ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaoweza kuwajibika wanapaswa kuwepo (ona 12.3.5).

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu watoto walio na mahitaji maalumu, mahitaji ya usalama, mpango wa Watoto na Vijana na vinginevyo vinapatikana katika sehemuĀ 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.