Wito Wangu kama Msaidizi wa Akidi ya Makuhani
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Ukuhani wa Haruni
Akidi za ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, Maktaba ya Injili.)
Akidi ya Makuhani
Vijana wanajiunga na akidi ya makuhani kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 16. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa makuhani kama wamejiandaa na wanastahili. Makuhani wana majukumu yaleyale sawa na ya mashemasi na walimu. Pia wanatayarisha sakramenti na kuhudumu kama akina kaka wahudumiaji. Kazi za ziada zimeainishwa katika Mafundisho na Maagano 20:53–59; 84:111. (Ona 10.1.3.2.)
Msaidizi
Wasaidizi wa akidi ya makuhani wanamsaidia rais wa akidi, askofu, katika majukumu yake. Hii inajumuisha juhudi za akidi zinazoongoza katika kushiriki kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa; kupata kumjua na kumhudumia kila mshiriki wa akidi, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mikutano ya akidi; kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi; kuwafundisha washiriki wa akidi majukumu yao ya ukuhani; na kupanga na kuendesha mikutano ya akidi (ona 10.4.2.) Urais wa akidi unapaswa kukutana mara kwa mara (ona 10.4.3).
Huduma na Shughuli
Uaskofu na viongozi wa akidi ya vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Hizi zinapaswa kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Zinapaswa kuwa na usawa kati ya maeneo manne ya ukuaji: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana, na kukusanya matoleo ya mfungo, zinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.