Wito Wangu kama Katibu wa Akidi ya Makuhani
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Ukuhani wa Haruni
Akidi za ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, Gospel Library.)
Akidi ya Makuhani
Wavulana hujiunga na akidi ya makuhani kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 16. Kama wamejitayarisha na kustahili, wanaweza pia kutawazwa kuwa makuhani. Makuhani wana majukumu sawa na yale ya mashemasi na walimu. Makuhani wanaweza pia kuhudumu kwenye sakramenti, kufanya ubatizo (ikijumuisha ubatizo wa hekaluni), na kuwatawaza makuhani wengine, walimu, au mashemasi ( ona Mafundisho na Maagano 20:46–52, 73–79; Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.1.3.3).
Katibu
Wakati makatibu katika akidi wanapokuwa wameitwa, wao ndio wanaotayarisha ajenda kwa ajili ya mikutano na kuandika mihutasari. Pia wanamsaidia karani wa kata au mshauri wa akidi kufuatilia mahudhurio. (Ona 10.4:2.)
Huduma na Shughuli
Askofu na viongozi wa akidi ya vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Hizi zinapaswa kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Zinapaswa kuwa na usawa kati ya maeneo manne ya ukuaji: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana, na kukusanya matoleo ya mfungo, zinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.