Msingi
Majukumu


mwanamke akiwafundisha watoto

Wito wangu kama Rais wa Darasa la Watoto

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Madhumuni ya Darasa la Watoto

Darasa la Watoto huwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; kujifunza kuhusu mpango Wake wa furaha; kuishi injili ya Yesu Kristo; na kuhisi, kutambua na kutenda juu ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wakati wa kujiandaa, kufanya na kuweka maagano matakatifu pale watoto wanaposhiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)

Rais na Urais

Urais wa Watoto unawasaidia wazazi wawaandae watoto kuingia na kuendelea kwenye njia ya agano. Hili ni moja ya majukumu yao muhimu zaidi. Rais anahudumu kama mjumbe wa baraza la kata. Yeye na washauri wake hukutana pamoja mara kwa mara na pia huwa na mikutano na askofu au mshauri wake aliyekabidhiwa. Urais husimamia mikutano ya Darasa la Watoto, kuhudumia watoto binafsi, walimu na viongozi, na mahitaji ya kiutawala ya Darasa la Watoto. (Ona 12.3:2.)

Madarasa na Muda wa Kuimba.

Ni fursa takatifu kufundisha watoto. Viongozi wa Watoto huwapenda na kuwafundisha watoto katika njia ya Mwokozi. Madarasa ya watoto hupangwa kulingana na umri na idadi ya walimu wanaopatikana (ona 12.1.3). Muda wa kuimba unawasaidia watoto wahisi upendo wa Baba wa Mbinguni na wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha (ona 12.1.4).

Mikutano na Mabaraza

Rais wa Watoto huwasilisha mahitaji ya watoto anapokutana na kushauriana na viongozi katika kata. Hii inajumuisha mikutano inayoendelea na askofu au mshauri aliyekabidhiwa, baraza la kata, urais na katibu, wazazi na wengine. (Ona 12.3:2.)

Walimu na Viongozi

Kufundisha watoto wa Mungu ni fursa takatifu. Urais wa Watoto hutoa msaada kwa walimu na viongozi wa Watoto wakati wa madarasa, chekechea na wakati wa kuimba (ona 12.3.5). Urais wa Watoto hupendekeza kwa uaskofu wanaume na wanawake kuhudumu katika miito ya Darasa la Watoto na chekechea.

Shughuli za Watoto

Viongozi wa shughuli za watoto hupanga shughuli za kufurahisha na kushirikisha ambazo husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Huduma na shughuli zinapaswa kujenga shuhuda, kuimarisha familia na kutoa fursa za kuwabariki wengine. Shughuli za watoto kwa ujumla hufanyika mara mbili kwa mwezi kwa watoto wa miaka 8–11. (Ona 12.3:6.)

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu watoto walio na mahitaji maalumu, mahitaji ya usalama, mpango wa Watoto na Vijana na vinginevyo vinapatikana katika sehemu 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.