Msingi
Majukumu


mwanamke akiwafundisha watoto

Wito wangu kama Mwalimu wa Darasa la Watoto

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Madhumuni ya Darasa la Watoto

Darasa la Watoto huwasaidia watoto wahisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha; waishi injili ya Yesu Kristo; na wahisi, watambue, na watende juu ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wakati wa kujiandaa, kufanya na kushika maagano matakatifu pale watoto wanaposhiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)

Mwalimu wa Darasa la Watoto

Kufundisha watoto wa Mungu ni fursa takatifu. Walimu wa Madarasa ya Watoto wanaitwa kufundisha na kuhudumia kundi la watoto wenye umri maalumu. (ona 12.3.5). Wanajifunza injili na kushiriki na watoto kile wanachojifunza. Walimu wanawahimiza watoto na familia zao kujifunza injili nyumbani. Wanawaalika watoto kushiriki kanisani kile wanachojifunza nyumbani (ona 12.2.1.2).

Darasa la Jumapili

Walimu wa Madarasa ya Watoto hufundisha kutoka Njoo, Unifuate. Wanafuata kanuni katika Kufundisha katika Njia ya Mwokozi na sura ya 17 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla. Wakati watu wazima wanapowafundisha watoto katika mazingira ya Kanisa, angalau watu wazima wawili wanaowajibika wanapaswa kuwepo (ona 12.3.5).

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu watoto walio na mahitaji maalumu, mahitaji ya usalama, programu ya Watoto na Vijana na vinginevyo vinapatikana katika sehemu ya 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.