Wito wangu kama Katibu wa Kigingi wa Darasa la Watoto
Majukumu
Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Dhumuni la Darasa la Watoto
Darasa la Watoto huwasaidia watoto wahisi upendo wa Baba yao wa Mbinguni; wajifunze kuhusu mpango Wake wa furaha; waishi injili ya Yesu Kristo; na wahisi, watambue na watende juu ya ushawishi wa Roho Mtakatifu. Darasa la Watoto pia ni wakati wa kujiandaa, kufanya na kushika maagano matakatifu pale watoto wanaposhiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 12.1.)
Katibu wa Kigingi wa Darasa la Watoto
Katibu wa Kigingi wa Darasa la Watoto anaunga mkono urais wa Kigingi wa Darasa la Watoto. Chini ya maelekezo ya rais wa wa Darasa la Watoto, katibu ana jukumu la kuandaa ajenda za mikutano ya urais, kuandika kumbukumbu katika vikao vya urais na kuweka kumbukumbu za kazi, kuweka kumbukumbu nyingine na kuandaa ripoti kama ofisi ya rais inavyoomba, kuusaidia urais kuandaa bajeti ya mwaka kwa ajili ya kikundi chao , kuwajibika kwa ajili ya gharama, na kutoa mafunzo kwa makatibu wa vikundi wa kata kama walivyopangiwa (ona 6.7.3).
Miongozo na Sera
Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi wa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu watoto walio na mahitaji maalumu, mahitaji ya usalama, programu ya Watoto na Vijana na vinginevyo vinapatikana katika sehemu ya 12.5 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.