Muungano wa Usaidizi
Majukumu


Picha
kundi la wanawake wakizungumza

Wito Wangu kama Katibu wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumui ya wito wako.

Dhumuni la Muungano wa Usaidizi

Muungano wa Usaidizi ni kikundi kitakatifu kilichoanzishwa kwa ajili ya wanawake watu wazima wote katika Kanisa. Muugano wa Usaidizi unawasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba dhumuni la Muungano wa Usaidizi ni “kuokoa nafsi na kuondoa mateso”—kutoa faraja ya Mwokozi (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 9.1).

Katibu wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi

Chini ya maelekezo ya rais wa Muungano wa Usaididizi katika Kigingi, katibu ana jukumu la kuandaa ajenda za mikutano ya urais, kuandika kumbukumbu katika vikao vya urais na kuweka kumbukumbu za majukumu, kuweka kumbukumbu zingine na kuandaa ripoti kadiri urais unavyoziomba, kuusaidia urais kuandaa bajeti ya mwaka kwa ajili ya kikundi chao, kuwajibika kwenye matumizi, na kutoa mafunzo kwa makatibu wa vikundi katika kata kama walivyopangiwa (ona 6.7.3).

Mikutano na Mabaraza

Katibu wa Muungano wa Usaidizi katika Kigingi anahudhuria mikutano ya urais na anahudumu pamoja na urais kwenye kamati ya uongozi ya watu wazima ya kigingi (ona 6.7.1.1).

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera vinapatikana katika sehemu ya 9.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha