Shule ya Jumapili
Majukumu


Picha
kundi la watu wakitabasamu

Wito wangu kama Katibu wa Shule ya Jumapili

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumui ya wito wako.

Kusudi la Shule ya Jumapili

Shule ya Jumapili husaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Inafanya hivi kwa kuwasaidia watoto wa Mungu kujifunza na kuishi injili ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 13.1).

Urais na Katibu

Rais wa Shule ya Jumapili anawajibika kusimamia ujifunzaji na ufundishaji wa injili nyumbani na Kanisani. Washauri wake wanamsaidia. Katibu anaweza kuusaidia urais kutunza kumbukumbu ya majukumu na mahudhurio (ona 13.2.2.2).

Madarasa ya Jumapili

Madarasa ya Shule ya Jumapili yanafanyika Jumapili ya kwanza na ya tatu ya mwezi. Ukubwa wa darasa utatofautiana kulingana na mahitaji ya kila kata (ona 13.3). Walimu wa Shule ya Jumapili hutumia maandiko, masomo yaliyopangwa ndani ya Njoo, Unifuate, na maneno ya manabii wa siku hizi kama nyenzo zao kuu za kufundishia.

Mafunzo Yanayolenga Nyumbani

Wazazi wanawajibika kuwafundisha injili watoto wao (ona 13.5). Walimu wa Shule ya Jumapili na viongozi wanawahimiza waumini kutafuta mwongozo wa kiungu wao wenyewe kuhusu jinsi gani ya kujifunza na kufundisha injili katika nyumba zao (ona 17.2).

Mikutano ya Baraza la Walimu

Katibu anaweza kumsaidia Rais wa Shule ya Jumapili kupanga na kuendesha mikutano ya baraza la walimu na mikutano ya baraza la walimu kwa ajili ya wazazi katika kila robo ya mwaka.

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya ulinzi wa watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo ya ziada ya Shule ya Jumapili inapatikana katika sehemu ya 13.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha