Wito Wangu kama Rais wa Akidi ya Walimu
Majukumu
Bwana anashukuru kwa ajili ya utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.
Lengo la Ukuhani wa Haruni
Akidi za Ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, Maktaba ya Injili.)
Akidi ya Walimu
Vijana wanajiunga na akidi ya walimu kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 14. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa walimu kama wamejiandaa na wanastahili. Walimu wana kazi zile zile kama za mashemasi. Pia wanatayarisha sakramenti na kuhudumu kama akina kaka wahudumiaji. Kazi za ziada zimeainishwa katika Mafundisho na Maagano 20:53–59; 84:111. (Ona 10.1.3.2.)
Rais
Majukumu ya rais wa akidi ya walimu yanajumuisha kuongoza juhudi za akidi katika kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa; kupata kumjua na kumhudumia kila mshiriki wa akidi, ikijumuisha wale ambao hawahudhurii mikutano ya akidi; kuwaimarisha waumini wapya na wanaorudi; kuwafundisha washiriki wa akidi majukumu yao ya ukuhani; na kupanga na kuendesha mikutano ya akidi (ona 10.4.2). Urais wa akidi unapaswa kukutana mara kwa mara (ona 10.4.3).
Baraza la Vijana
Rais wa akidi ya walimu ni mshiriki wa baraza la vijana la kata. Lengo la baraza hili ni kuwasaidia vijana kuwaleta wengine kwa Yesu Kristo na kusaidia kutimiza kazi ya wokovu na kuinuliwa. Askofu anasimamia baraza la vijana la kata. (Ona 10.4:4.)
Huduma na Shughuli
Uaskofu na viongozi wa akidi ya vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Haya yanapaswa kusaidia kutimiza kazi ya wokovu na kuinuliwa. Zinapaswa kuwa na usawa kwenye maeneo manne ya ukuaji: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)
Miongozo na Sera
Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana, na kukusanya matoleo ya mfungo, zinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.