Akidi za Ukuhani wa Haruni
Majukumu


kundi la wavulana

Wito wangu kama Katibu wa Akidi ya Walimu

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Ukuhani wa Haruni

Akidi za ukuhani wa Haruni zinawasaidia wavulana kufanya na kuyashika maagano matakatifu na kuzidisha kwa kina uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Dhumuni la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani kufanya kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 10.1, Gospel Library.)

Akidi ya Walimu

Wavulana wanaijunga na akidi ya walimu kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha umri wa miaka 14. Wakati huu wao pia wanastahili kutawazwa kuwa walimu kama wamejiandaa na wanastahili. Walimu wana kazi zile zile kama mashemasi. Pia wanatayarisha sakramenti na kuhudumu kama akina kaka wahudumiaji. Kazi za ziada zimeainishwa katika Mafundisho na Maagano 20:53–59; 84:111. (Ona 10.1.3.2.)

Katibu

Wakati makatibu katika akidi wanapokuwa wameitwa, wao ndio wanaotayarisha ajenda kwa ajili ya mikutano na kuandika mihutasari. Pia wanamsaidia karani wa kata au mshauri wa akidi kufuatilia mahudhurio. (Ona 10.4:2.)

Huduma na Shughuli

Uaskofu na viongozi wa akidi za vijana, wakisaidiwa na washauri, wanapanga huduma na shughuli. Haya yanapaswa kusaidia kukamilisha kazi ya wokovu na kuinuliwa. Shughuli zinapaswa kuwa na uwiano miongoni mwa maeneo manne ya ukuaji binafsi: kiroho, kijamii, kimwili na kiakili. (Ona 10.2.1.3.)

Miongozo na Sera

Miongozo ya ziada na sera, ikijumuisha kuwasaidia wavulana wenye ulemavu, kupokea nembo za Watoto na Vijana na kukusanya matoleo ya mfungo, vinapatikana katika sehemu ya 10.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.