Music
Majukumu


Picha
mwanamke akiongoza kwaya

Wito Wangu kama Mwendeshaji wa Kwaya katika Kata

Majukumu

Bwana anashukuru kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Madhumuni ya Muziki katika Kanisa

Muziki mtakatifu unaongeza imani katika Yesu Kristo. Unamwalika Roho na unafundisha mafundisho. Pia unatengeneza hisia za staha, unawaunganisha waumini, na unatoa njia ya kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Bwana alitamka, “Kwani nafsi yangu hufurahia nyimbo za moyoni” (Mafundisho na Maagano 25:12). (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 19.1.)

Mwendeshaji wa Kwaya katika Kata

Mwendeshaji wa kwaya katika kata huwasaidia waumini wa kata waongeze imani na kumwabudu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia muziki mtakatifu. Wanapendekeza muziki kwa ajili ya kwaya ya kata, kuendesha mazoezi ya kwaya, na huongoza kwaya katika mikutano ya Kanisa (ona 19.4.3.3).

Kwaya za Kata

Kwaya za Kanisa huleta utukufu kwa Mungu, kuunganisha na kuwajenga waumini wa Kanisa, na kuleta shangwe kwa washiriki na mikusanyiko. Kwaya inahimizwa kutumia nyimbo za Kanisa, ambazo zinamwalika Roho na kusaidia washiriki wa kwaya na mikusanyiko kujifunza injili (ona Nyimbo za Dini,381–83). Kwaya za Kanisa zinaweza pia kuimba chaguzi zingine za muziki mtakatifu. Chaguzi zote za muziki zinapaswa kufundisha injili kwa nguvu na uwazi. (Ona 19.3.)

Miongozo na Sera

Mazoezi ya kwaya kwa kawaida hayazidi saa moja. Kwa sera na miongozo ya ziada, kama vile kupatikana kwa muziki, matumizi ya vifaa vya nyumba ya mikutano kwa ajili ya mazoezi, au kwaya za jamii, ona sehemu ya 19.7 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha