Wasichana
Majukumu


Picha
wasichana wakitabasamu

Wito Wangu Kama Katibu wa Wasichana

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la wasichana

Kikundi cha Wasichana huwasaidia mabinti wapendwa wa Mungu wajiandae kurudi katika uwepo Wake. Kinawasaidia wasichana wafanye na washike maagano matakatifu na kuzidisha uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake. Katika madarasa yao, wasichana wanawatumikia wengine, wanatimiza majukumu ya kimaagano, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 11.1.1.)

Katibu

Katibu wa Wasichana humsaidia rais katika kuandaa ajenda, kuandika kumbukumbu, na kufuatilia majukumu ya mikutano ya urais. Pia anawaelekeza makatibu wa darasa, anawasaidia watunze kumbukumbu za mahudhurio, na kuusaidia urais wa Wasichana katika kuandaa bajeti na kuwajibika kwa matumizi (ona 11.3.3).

Madarasa ya Jumapili

Uaskofu na viongozi watu wazima wa Wasichana kwa sala wanaamua jinsi ya kupanga madarasa kulingana na umri. Wanazingatia fursa za uongozi kwa ajili ya wasichana. Kila darasa, bila kujali ukubwa, linapaswa kuwa na rais na, pale inapowezekana, mshauri mmoja au wawili na katibu (ona 11.1.3).

Huduma na Shughuli

Urais wa darasa, ukiungwa mkono na viongozi watu wazima, hupanga huduma na shughuli zinazojenga shuhuda, kuimarisha familia, kukuza umoja wa darasa, na kutoa fursa za kuwabariki wengine (ona 11.2.1.3). Huduma na shughuli ni fursa ya kuwakusanya vijana na kushiriki shangwe ya kuishi injili na kushiriki katika kazi kuu ya Bwana.

Miongozo na Sera

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto na vijana lazima wakamilishe mafunzo ya Ulinzi kwa Watoto na Vijana ndani ya mwezi mmoja baada ya kukubaliwa (ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Miongozo na sera kuhusu wasichana wenye ulemavu, nembo za vijana, na mengine zaidi yanapatikana katika sehemu ya 11.6 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Chapisha