Akidi ya Wazee
Majukumu


kundi la wanaume wakiwa wamekaa pamoja

Wito Wangu Kama Katibu wa Akidi ya Wazee

Majukumu

Bwana ana shukrani kwa utayari wako wa kuhudumu katika Kanisa Lake. Hapa chini ni muhtasari wa majukumu ya wito wako.

Dhumuni la Akidi ya Wazee

Ukuhani wa Melkizedeki huwasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurudi kwenye uwepo Wake. Washiriki wa akidi ya wazee hufanya kazi pamoja ili kusaidia kukamilisha kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Wanawatumikia wengine, wanatimiza wajibu wa ukuhani, wanajenga umoja, na wanajifunza na kuishi mafundisho (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 8.1).

Katibu wa Akidi ya Wazee

Urais wa akidi ya wazee na katibu hukutana mara kwa mara. Majukumu ya katibu yanaweza kujumuisha kuandaa ajenda, kuandika kumbukumbu, kufuatilia majukumu, kuratibu usaili wa wahudumiaji, kuandaa na kuwasilisha ripoti za mahudhurio, na kusaidia kuandaa bajeti (ona. 8.3.4).

Mikutano ya Jumapili

Akidi za wazee hukutana Jumapili ya pili na ya nne ya mwezi ili kukuza imani, kujenga umoja, na kuimarisha familia na nyumba. Urais wa akidi ya wazee kwa sala huchagua jumbe kutoka kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni zaidi ili kujadili kulingana na mahitaji ya washiriki (ona 8.2.1.2).

Huduma na Shughuli

Urais wa akidi ya wazee wanaweza kupanga shughuli za kuwaimarisha washiriki wa akidi na kuwapa fursa za kuhudumu pamoja (ona 8.2.1.3).