Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 40


Sehemu ya 40

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko Fayette, New York, 6 Januari 1831. Kabla ya kumbu kumbu ya ufunuo huu, Historia ya Nabii inaeleza, “Wakati James Covel alipokataa neno la Bwana, na kurejea kwenye kanuni na watu wake wa awali, Bwana alinipa mimi na Sidney Rigdon ufunuo ufuatao” (sehemu ya 39).

1–3, Woga wa mateso na shughuli za ulimwengu husababisha kukataliwa kwa injili.

1 Tazama, amini ninawaambia, kwamba moyo wa mtumishi wangu James Covel ulikuwa safi mbele zangu, kwani aliagana nami kuwa atatii neno langu.

2 Na akalipokea neno kwa furaha, na moja kwa moja shetani akamjaribu; na woga na mateso na shughuli za ulimwengu zikamsababisha yeye kulikataa neno.

3 Kwa hiyo basi alivunja agano langu, na imebaki kwangu mimi kufanya kwake nilionalo kuwa ni jema. Amina.