Mikutano ya Ibada ya Ulimwenguni Kote
Kuishi kwa Kusudi: Umuhimu wa “Kusudi Halisi”


Kuishi kwa Kusudi: Umuhimu wa “Kusudi Halisi”

Jioni na Ndugu RandallL. Ridd Mkutano wa Ibada Duniani Kote kwa Vijana Wazima • Januari 11, 2015 • Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho

Ni fursa ya ajabu jinsi gani kuwa nanyi jioni ya leo. Ni heshima kubwa kwa mke wangu nami kuwa hapa jioni hii. Nilifikiria itakuwa jambo la kufurahisha kwamba simu yangu ijue kwamba nilikuwa na safari hii kuja Rexburg kwenye kalenda yangu leo. Iliniambia jinsi hali ya hewa itakavyokuwa na ikanipa orodha ya hoteli na migahawa iliyopo jijini. Simu yangu pia iliniambia kuhusu vivutio vingi vinavyopatikana Rexburg wikiendi hii.

We! Sasa ninapofikiria kuhusu hili---haikuorodhesha hotuba yangu kama mmojawapo ya vivutio. Nadhani hivyo ndivyo unavyojua kwamba ni simu ya kisasa!

Hata ingawa smartphone yako haikupendekeza, kila mmoja wenu amechagua kutumia saa moja ya muda wenu kuwa pamoja nami usiku wa leo---lisaa limoja ambalo kamwe hamtalipata tena. Kwa hiyo, ninahisi wajibu mkubwa kuifanya kuwa ya maana sana. Lakini pia ninajua kwamba kile ninachosema hakitakuwa muhimu kama kile Roho anachowafundisha, na hiyo itakuwa tu na thamani kama msimamo wenu wa kutenda juu ya shawishi hizo.

Nafikiri utakubaliana na mimi kwamba huu ni wakati wa ajabu kuwa hai. Wanasosiolojia waliita kizazi changu Baby Boomers, ingawa neno hili halitumiki tena; wamekiita kizazi kijacho, kizazi  X, na wamewaita ninyi kizazi  Y, ama Millennials. Mkijulikana kwa urahisi wenu wa asili wa teknolojia na jinsi mlivyokumbatia mitandao wa kijamii, nyinyi ni werevu zaidi na mlioelimika zaidi kuliko vizazi vilivyopita. Sifa hizi haziwafanyi tu kuzidi kuwa na thamani kubwa katika jamii ya leo lakini pia katika kufanya kazi ya Bwana.

Mna chaguo zaidi na fursa zaidi kuliko wakati wowote uliopita. Kama mambo mengi katika maisha, hizi zote ni baraka na laana. Chaguo nyingi sana, na hofu ya kufanya maamuzi mabaya, mara nyingi husababisha “kiharusi cha maamuzi,” ambayo ni moja ya changamoto za kizazi chenu. Ni vigumu zaidi kulenga jambo fulani kuliko wakati wowote uliopita! Na teknolojia, punde unaponunua kitu fulani, uwezekano kwamba kitakuwa kimepitwa na wakati punde tu unapoondoka dukani. Watu wengi wanaogopa kufanya kitu chochote kwa sababu wanashuku kama chaguo bora lipo karibu kuja. Hivyo basi wanasubiri---na mwishowe hawachagui chochote. Katika hali hii ya kutoonyesha hisia wanaweza kulengwa kirahisi na mambo ya kuangamiza. Kiuwasumu chake, ndugu na akina dada, ni kile ningependa kukizungumzia jioni hii---kuishi kwa kusudi: umuhimu wa kusudi halisi.

I.   Kusudi

Fikiria kwa muda uko katika mashuaokozi kwenye bahari, bila chochote bali mawimbi yanayo vuma kila upande, kwa umbali ambao unaoweza kuona. Mashua imeandaliwa na makasia, lakini ni mwelekeo upi unge kufuata? Sasa fikiria umeona nchi kavu kwa mbali. Sasa unajua mwelekeo ambao lazima uende. Je, kuona nchi kavu kunakupatia vyote motisha na kusudi? Watu ambao hawana dhana wazi ya kusudi ni waeleaji. Waeleaji huruhusu mawimbi ya dunia kuamua wapi watakokwenda.

Leo Tolstoy

Maisha ya mwandishi mkuu wa Kirusi Leo Tolstoy, mwandishi wa Vita na Amani, yanaonyesha wazo hili. Leo Tolstoy alikuwa na ujana mgumu. Wazazi wake walifariki alipokuwa na umri wa miaka karibu 13. Akasomeshwa na kaka zake njia za pombe, kamari, na uasherati, Leo alikuwa hatii bidii katika masomo yake. Akiwa na umri wa miaka 22, alianza kuhisi kwamba maisha yake yalikosa kusudi la kweli la kuishi na akaandika katika jarida lake, “Ninaishi kama mnyama.” Miaka miwili baadaye aliandika, “Nina umri wa miaka 24 na bado sijafanya chochote.” Kutokuridhika kwa Tolostoy kulimpa motisha kuanza jitihadi ya kimaisha kutafuta, hasa kupitia kujaribu na kukosa, kusudi la maisha yake--- kwa nini. Kabla hajafa akiwa na umri wa miaka 82, alihitimisha katika jarida lake, “Maana yote na furaha ya maisha,’  … imo katika kutafuta ukamilifu na kuelewa mapenzi ya Mungu” 1---na nitaongeza kufanya mapenzi ya Mungu.

Imesemwa kwamba siku mbili za muhimu sana maishani mwako ni siku uliyozaliwa na siku unapofahamu kwa nini ulizaliwa.2 Kwa sababu tuna injili, hatuna haja ya kutumia maisha yetu yote kujaribu kutafuta kusudio lake. Badala yake, tunaweza kulenga kwenye kutimiza kusudi hilo.

Katika Mathayo 5:48 tunaosoma, “Muwe wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Ninafikiria kila mmoja wetu ana hulka ya kutamani kuimarika. Lakini kwa sababu sote hufanya makosa, wengi wetu tunashawishika kwamba lengo la ukamilifu haliwezifikiwa. Na huenda likawa---kama haingekuwa ni kwa sababu ya Upatanisho. Dhabihu ya Mwokozi wetu inawezesha ukamilifu. “Ndio, mje kwa Kristo na mkamilishwe ndani yake, na mjinyime uovu wote; na ikiwa mtajinyima uovu wote, na kumpenda Mungu kwa uwezo wenu wote, akili na nguvu zenu zote, ndipo neema yake inawatosha, kwamba kwa neema yake mnaweza kuwa wakamilifu katika Kristo” (Moroni 10:32; mkazo umeongezwa).

Mwokozi wetu ametupa tumanini ambalo linatushawishi kuwa kama Baba wetu wa Mbinguni. Mnajua, kama vile Leo Tolstoy alivyokuja kujua, kwamba kuna furaha katika safari ya ukamilifu. Kusudi kuu huja katika maisha yenu wakati mnapolifanya kuwa jukumu lenu kufuata mapenzi ya Bwana.

Mzee Tad R. Callister aliuliza: “[Na] kwa nini ni muhimu sana kuwa na ono sahihi la hitimisho hili tukufu la uungu ambalo maandiko na mashahidi wengine wanashuhudia kwa wazi? Kwa sababu pamoja na ongezeko la maono huja ongezeko la motisha Zaidi.” 3

Misheni

Nilipokuwa kijana, nilikuwa karibu niamue kutokwenda misheni. Baada ya mwaka mmoja katika chuo na mwaka katika jeshi, nilikuwa na kazi mzuri katika hospitali ya mtaa kama fundisanifu wa X-ray. Siku moja Dkt. James Pingree, mmoja wa madaktari wapasuaji katika hospitali, alinialika kula chakula cha mchana. Katika mazungumzo yetu, Dkt. Pingree aligundua kwamba sikuwa ninapanga kuhudumu misheni na akauliza kwa nini? Nilimwambia kwamba nilikuwa na umri mkubwa kiasi na huenda ilikuwa imechelewa. Hapo hapo aliniambia kwamba hiyo hahikuwa sababu nzuri sana na kwamba alikuwa ameenda misheni yake baada ya kumaliza shule ya Udaktari. Kisha alitoa ushuhuda wake wa umuhimu wa misheni yake.

Ushudhuda wake ulikuwa na ushawishi mkubwa kwangu, na ulinisababishia kuomba ambavyo sijawahi kuomba kabla---na kwa dhamira halisi. Ningeweza kufikiria sababu nyingi za kutoenda misheni. Nilikuwa na haya, kwa kiwango cha juu sana kwamba wazo la kutoa mazungumzo ya kuagana katika mkutano wa Sakramenti lilikuwa sababu ya kutosha ya kutokwenda. Nilikuwa na kazi ambayo niliipenda. Nilikuwa na uwezekano wa kupata msaada wa masomo ambao haungekuwepo baada ya misheni. Muhimu kabisa, nilikuwa na mchumba ambaye aliningojea nilipokuwa katika jeshi---na nilijua hangengojea miaki miwili mingine! Niliomba na kuomba ili kupata hakikisho kwamba sababu zangu zilikuwa halali na nilikuwa na sahihi.

Kwa kukatishwa tamaa kwangu, sikuweza kupata jibu rahisi la ndio-ama-la nililokuwa ninatumahi. Kisha wazo lilinijia, “Bwana anataka ufanye nini?” Ilinibidi nikubali kwamba alitaka nihudumu misheni, na huu ukawa wakati wa uamuzi mwisho maishani mwangu. Nilikuwa nifanye kile mimi nilitaka kufanya ama nifanye mapenzi ya Bwana? Hili ni swali tungefanya sote vyema kujiuliza mara nyingi. Ni mpangilio mzuri kiasi gani kwa kila mmoja wetu kuanzisha mapema katika maisha yetu. Mara nyingi tuna mtazamo wa “Nitaenda unakotaka niende na kufanya unachotaka nifanye, Bwana mpendwa – ilimradi tu ni mahali ninataka kwenda na kile ninachotaka kufanya.”

Kwa shukrani, nilichagua kwenda misheni na nilitumwa kuhudumu Misheni ya Mexico North. Ili kupunguza shaka baadhi yenu huenda mkawa mnahisi---ninaweza kuwaambia kwamba mchumba wangu hakuningojea, bali nilimuoa hata hivyo! Yeye ni baraka kubwa katika maisha yangu. Nikijua kusudi la maisha yetu ni kuwa kama Baba yetu wa Mbinguni, nimegundua kwamba hakuna chuo kikuu cha maana kaidi kuliko kile cha kuwa katika ndoa na kuwa na familia kutufundisha juu ya upendo wa Mungu kwa watoto Wake. Nikiwa ninajua ninachokijua sasa, ningeyafanya yote niwezayo ili niweze kuingia katika chuo kikuu hicho ningalikuwa ninyi. Ninaelewa kwamba kujisajili kwa mapema kumefunguliwa hivi sasa.

II. Kusudi Halisi

Wakati mwana wetu alikuwa anajifunza kuongea, alikuwa na udadisi usiotosheleka. Katika msamiati wake finyu wa kuzungumza neno alilopenda lilikuwa “Kwa nini?” kama Nikisema, “Ni saa ya kujitayarisha kulala,” angejibu na “Kwa nini?”

“Ninaenda kazini.”

“Kwa Nini?”

“Tuseme sala zetu.”

“Kwa Nini?”

“Ni saa ya kwenda kanisani.”

“Kwa Nini?”

Ilifurahisha sana---mara 500 ya kwanza alipoisema. Lakini hata baada ya uzuri kuisha na ikawa kiasi inachosha, nilikuwa na shukurani kwa ukumbusho wa kila mara kuchunguza kwa nini iliyonyuma ya (hasa) kila kitu nilichokifanya.

Sina uhakika kuna umuhimu mwingi katika herufi  Y kama jina la kizazi chenu, lakini ninafikiri kuna thamani katika kujifikiria wenyewe kama kizazi cha “kwa nini?” Ni muhimu, katika dunia ya sasa, kuwa na kusudi kuhusu ni kwa nini unafanya kile ufanyacho.

Kuishi na kusudi halisi kunamaanisha kuelewa “sababu” na kuwa na ufahamu wa nia ya vitendo vyetu. Socrates alisema, “Maisha yasiyochunguzwa hayana thamani ya kuishi.” 4 Tafakari jinsi unavyotumia wakati wako, na jiulize kila mara, “Kwa nini?” Hii itakusaidia kukuza uwezo wa kuona kupita wakati wa sasa. Ni bora zaidi kutazama mbele na kujiuliza, “Kwa nini ningefanya hivyo?” kuliko kuangalia nyuma na kusema, “Kwa nini, we, kwa nini nilifanya hivyo?”

Nyota

Nilijifunza umuhimu wa kusudi halisi nilipokuwa mwanafunzi kijana wa seminari. Mwalimu wetu alitupa changamoto ya kusoma Kitabu cha Mormoni. Ilikusaidia kupima maendeleo yetu, alitengeneza chati iliyo na majina yetu kwa upande moja na vitabu vikiwa vimeorodheshwa upande wa juu. Kila wakati unaposoma kitabu, nyota iliwekwa kando ya jina lako. Mara ya kwanza sikutia bidii sana kusoma, na haikuchukua muda mrefu kabla ya kujikuta nikiwa nyuma zaidi na zaidi. Nikiwa nimeshawishiwa na hisia ya aibu na nafsi yangu asili ya ushindani, nilianza kusoma. Kila wakati nilipopata nyota, nilijisikia vizuri. Na nyota zaidi nilizokuwa nazipata, ndivyo nilitiwa motisha zaidi ya kusoma---katikati ya madarasa, baada ya shule, katika kila dakika ya ziada.

Hii ingekuwa hadhithi nzuri kama ningeweza kuwaambia nilimaliza wa kwanza katika darasa---lakini sikumaliza wa kwanza. (hata hivyo, sikuwa wa mwisho, licha ya hayo.) Lakini unajua nilipata nini kwa kusoma Kitabu cha Mormoni? Ninajua mnafikiria “ushuhuda”, je hamfikirii hivyo? … Lakini sikupata ushuhuda. Nilipata nyota. Nilipata nyota kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa kwa nini nilikuwa ninasoma. Hilo ndilo lilikuwa kusudi langu halisi .

Moroni alikuwa wazi alipoelezea jinsi ya kupata kujua kama Kitabu cha Mormoni ni cha kweli: “Na Mtakapopokea vitu hivi, ningewashauri kwamba mngemwuliza Mungu, Baba wa Milele, katika jina la Kristo, ikiwa vitu hivi ni vya kweli; na ikiwa mtauliza na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu” (Moroni 10:4; mkazo umeongezwa ).

Nikitazama nyuma, ninaweza kuona kwamba Bwana alikuwa na haki kabisa nami. Kwa nini ningetarajia kupata zaidi ya kile nilichokuwa ninatafuta? Sikuwahi kamwe kusimama na kujiuliza kwa nini nilikuwa ninasoma Kitabu cha Mormoni. Nilikuwa nakienda bila malengo wala mwelekeo, nikiruhusu motisha za kidunia kuniongoza, sana kugundua kwamba nilikuwa nimesoma kitabu sahihi kwa sababu isiyosahihi. Kusudi halisi ni kufanya kitu sahihi kwa sababu sahihi.

Haikuwa hadi miaka mingi baadaye, nilipokuwa ninajitahidi kuamua kama niende misheni au la, ndipo nilisoma Kitabu cha Mormoni na kusudi halisi. Kama nilikuwa naenda kutumia miaka miwili nikitoa ushuhuda wa kitabu hicho, kwanza nilihitaji kuwa na ushuhuda.

Ninajua kwamba Kitabu cha Mormoni kinatimiza kusudi lake tukufu la kushuhudia juu ya maisha na huduma ya Yesu Kristo kwa sababu nimekisoma na kusudi hasili.

Fumbo la Machungwa

Ningependa kushiriki fumbo la kisasa ambalo nitaliita “Fumbo la Machungwa.” Mnaposikiliza, zingatia kile hadithi hii inakufundisha kuhusu uwezo wa kusudi halisi.

Kulikuwa na mvulana aliyekuwa na matarajio kufanya kazi kwenye kampuni kwa sababu ililipa vizuri na ilikuwa ya kifahari sana. Alitayarisha muhtasari wake na akawa na mahojiani kadha. Hatimaye alipewa cheo cha chini cha kuanzia. Kisha aligeuza matarajio yake kwa lengo lake linalofuata, kuongezwa mamlaka---cheo cha msimamiaji ambacho kingempa ufahari zaidi na malipo zaidi. Basi alikamilisha majukumu aliyopewa. Alikuja mapema asubuhi kadha na alichelewa ili bosi aweze kumwona akifanya kazi masaa mengi.

Mvulana yule alikasirika sana na alimwendea bosi wake na kudai maelezo.

Bosi mwenye hekima alisema, “Kabla sijajibu swali lako, je, unaweza kunifanyia fadhila ?”

“Ndio, hakika,” alisema mfanyikazi.

“Unaweza kwenda dukani na ununue machungwa kadha? Mke wangu anayahitaji.”

Mvulana alikubali na akaenda dukani. Aliporudi, bosi alimuliza, “Ulinunua aina gani ya machungwa?”

“Sijui,” mvulana yule alijibu. “Ulisema tu ninunue machungwa, na haya ni machungwa. Haya hapa.”

“Yaligarimu kiasi gani ?” bosi aliuliza.

“Kwa kweli, sina uhakika,” lilikuwa jibu. “Ulinipa dola 30. Hii hapa risiti yako, na hii hapa pesa iliyobaki.”

“Asante,” alisema bosi. “Sasa tafadhali keti chini na usikilize kwa makini.”

Kisha bosi alimwita mfanyikazi aliyekuwa amepandishwa cheo na akamuliza afanye kazi ile ile. Alikubali mara moja na akaenda dukani.

Aliporudi, bosi aliuliza, “Aina gani ya machungwa uliyonunua?”

“Vyema,” alijibu, “duka lilikuwa na aina nyingi---kulikuwa na machungwa ya navel, Machungwa ya Valencia, blood oranges, machenza, na mengineo, na sikujua gani ya kununua. Lakini nilikumbuka ulisema kwamba mke wako aliyahitaji machungwa, hivyo basi nilimpigia simu. Alisema alikuwa na karamu na kwamba atatengeneza maji ya machungwa. Basi nikamwuliza muuzaji ni yapi kati ya machungwa haya yote yangetengeneza maji ya machungwa bora zaidi. Alisema chungwa la Valencia lilikuwa na maji mengi matamu, basi hayo ndiyo niliyoyanunua. Niliyapeleka nyumbani kwako nilipokuwa njiani nikirudi ofisini. Mke wako alifurahia sana.”

“Yaligharimu pesa ngapi?” bosi aliuliza.

“Vyema, hilo lilikuwatatizo lingine. Sikujua ninunue mangapi, basi nilimpigia mke wako tena na nikamuuliza ni wageni wangapi alikuwa anawatarajia. Alisema 20. Basi nikamuuliza muuzaji ni machungwa mangapi yangehitajika kutengeneza maji ya machungwa ya kutosha watu 20, na yalikuwa mengi. Basi nikamuuliza muuzaji kama angeweza kunipunguzia, na alinipa! Machungwa haya kwa kawaida hugharimu senti 75 kila moja, lakini nililipa senti 50. Hii hapa pesa iliyobaki na risiti.

Bosi alitabasamu na kusema, “Asante; unaweza kwenda .”

Aligeukia upande kwa mvulana yule aliyekuwa anatazama. Mvulana alisimama, akaangusha ghafula mabega yake na kusema, “Ninaona unachomaanisha,” alipokuwa anatembea akiwa amevunjika moyo nje ya ofisi.

Ni nini kilichokuwa tofauti kati ya wavulana hawa wawili? Wote wawili waliombwa wakanunue machungwa, na walinunua. Huenda ukasema mmoja alienda hatua zaidi, ama alikuwa na ufanisi zaidi, ama alizingatia zaidi maelezo kwa kina. Lakini tofauti kubwa kabisa ilihusu kusudi halisi, badala tu kupitia kwenye vitendo. Mvulana wa kwanza alitiwa motisha na pesa, cheo, na ufahari. Mvulana wa pili alivutiwa na kusudi zito la kumfurahisha mwajiri wake na uamuzi wa ndani kuwa mfanyikazi bora angeweza kuwa ---na matokeo yalikuwa wazi.

Mnawezaje kutumia fumbo hili katika maisha yenu? Jinsi gani juhudi zenu katika familia zenu, shuleni, kazini, na Kanisani, zinaweza kuwa tofauti kama daima mngetafuta kumfurahisha Mungu na kufanya mapenzi Yake, ukisukumwa na upendo wako kwake?

III. Matumizi

Kuepuka Vishawishi---Umuhimu wa Msisitizo

Ni mara ngapi umeketi katika kompyuta kufanya kazi ya nyumbani ama zoezi la kazini, ambapo ghafla kunatokea tangazo la viatu, kama tu vile ulivyokuwa unavitafuta jana? Kisha, unapotafuta katika duka la mtandao, unagundua kwamba baadhi ya marafiki zako wako kwenye tovuti, basi uananza kuwasiliana nao. Kisha unapokea ilani kwamba rafiki ameandika jambo fulani kwenye Facebook, na lazima tu uangalie ni nini. Kabla haujajua, umepoteza wakati muhimu na kusahau ni kwa nini ulikuwa kwenye kompyuta mwanzoni. Basi mara nyingi sisi hupotoka wakati tunapaswa kuwa tumetenda. Vishawishi hukuibia wakati wako ambao ungewekezwa katika kufanya mema. Uwezo wa kuwa na msisistizo unatusaidia kuepuka vishawishi.

Ninajua ninyi nyote hufurahia kufanya majaribio. Basi, usiku wa leo nitawapa jaribio la haraka la uwezo wenu wa kuwa na msisitizo. Mtaona timu mbili: moja ikivalia rangi nyeupe na ingine ikivalia rangi nyeusi. Watapitisha mpira wa kikapu, na mimi ningependa mhesabu tu idadi ya pasi timu ya rangi nyeupe itafanya.

[Video ya mtihani wa ufahamu ilionyesha.]

Ni pasi ngapi mmehesabu?

Inua mkono kama ulihesabu pasi  19, Ni wangapi wamehesabu pasi  20,Ni wangapi wamehesabu pasi   21?Ni wangapi wamehesabu pasi  22?

Jibu sahihi ni 21.

Wote waliopata sahihi kama 21, inueni mikono yenu. Sasa acheni mikono yenu juu ikiwa pia mliona mwanamke mkongwe akitembea, kisha akitembea kwa kudensi sakafuni. Sasa achene mikono yenu juu ikiwa muliona mpiganaji wa kininja akimbadilisha mmoja wa wachezaji ya rangi nyeusi. Je, muliona wachezaji kwenye timu ya rangi nyeusi wamevalia kofia? Tazameni tena, na mlenge kwenye kitu ambacho hamkukiona mara ya kwanza.

Sasa tazama kwa mara ingine, muweke msisitizo kwenye kitu ambacho haukiona mara ya kwanza.

(Video ya mtihani wa ufahamu inachezwa tena.)

Tutaiweka hii video baadaye katika mitandao ya kijamii

Msisitizo wetu maishani ni muhimu sana. Kama vile jaribio hili linavyoonesha, kwa kawaida sisi hupata kile tunachotafuta. Au, kama vile maandiko yanavyosema, “tafuta, na utapata” (Luka11:9).

Kama tumelenga vitu vya duniani, tunaweza kupoteza dunia mzima ya kiroho ambayo imetuzunguka . Huenda tusiweze kutambua ushawishi wa kiroho ambao Roho Mtakatifu ana hamu kubwa ya kutupa ili kuongoza maisha yetu na kuwabariki wengine. Kinyume na hayo, kama tukilenga vitu vya Roho na kile ambacho ni “chema, chenye kupendeza, au chenye taarifa njema au chenye kustahili sifa” ( Makala ya Imani 1:13), ndipo tunakuwa na uwezekano mdogo wa kuchepushwa na majaribu na vivutio vya ulimwengu. Njia mzuri ya kuepuka vivutio ni kuwa na msisitizo uliowekwa imara kwenye kusudi ltu na kwa hamu kubwa iliyofungamana katika jambo zuri. Uwe makini kwa msisitizo wako---usitumie muda ukisisitizia katika kupanda mlima na kugundua kwamba umepanda mlima ambao sio.

Uwezo wa Vitu Vidogo

Miaka thelathini na mitano baada ya “kubadilisha msisitizo wangu na kuamua kuhudumu misheni, mwanangu alinihimiza kutembelea Mexico pamoja naye na, kwa kutumaini, tuwapate baadhi ya watu niliokuwa nimefundisha. Tulihudhuria mkutano wa sakramenti katika kijiji ndogo ambako nilianza misheni yangu, nikiwa nafikiria ningeweza kutambua mtu---angalau mmoja. Baada ya mkutano, tulimuuliza askofu kama angetambua yeyote kutoka kwa orodha yangu ya watu tuliowafundisha na kuwabatiza. Hamna hata mmoja. Alielezea kwamba alikuwa tu mshiriki kwa miaka mitano. Alipendekeza tuzungumze na mtu mwingine ambaye alikuwa mshiriki kwa miaka 27---bado kubahatisha tu, bali ilifaa kujaribu. Nilipitia orodha yangu naye bila mafanikio hadi tulipofikia jina la mwisho: Leonor Lopez de Enriquez.

“ Aha, ndio” alisema. “Familia hii iko katika kata nyingine, lakini wao huudhuria jengo hili. Mkutano wao wa sakramenti unafuatia; wangekuwa hapa hivi punde.”

Tulihitajika kungoja karibu dakika 10 tu kabla Leonor alipofika akitembea kuingia katika jengo. Ingawa sasa akiwa katika miaka yake za 70, nilimtambua mara moja, na alinitambua mimi. Tulikumbatiana kwa muda mrefu tukitokwa machozi .

Alisema, “Tumeomba kwa miaka 35 kwamba ungerudi ili tuweze kukushukuru kwa kuleta injili kwa familia yetu.”

Wanafamilia wengine walipokuwa wanaingia katika jengo, tulikumbatiana na kutokwa . Machozi. Kutoka kona ya jicho langu, niweza kumwona mwanangu akisimama pamoja na wamisionari wawili, ambao walikuwa wanapanguza machozi yao kwa tai zao.

Ilikuwa jambo la kufurahisha, tulipohudhuria mkutano wa sakramenti, kugundua kwamba askofu alikuwa mmoja wa wana wa Leonor, mpiga kinanda alikuwa mjukuu, mwelekezaji wimbo alikuwa mjukuu, kulikuwa na baadhi ya wavulana katika Ukuhani wa Haruni ambao walikuwa wajukuu, mmoja wa mabinti alikuwa ameolewa na mshauri katika urais wa kigingi. Binti mwingine alikuwa ameolewa na askofu wa kata iliyokuwa karibu. Wengi wa watoto wa Leonor walienda misheni, na sasa wajukuu pia wamehudumu misheni.

Tulipata kujua kwamba Leonor alikuwa mmisionari bora zaidi kuliko tulivyo kuwa. Leo, watoto wake wanakumbuka kwa shukrani juhudi zake bila kuchoka kuwafundisha injili: umuhimu wa zaka, mahekalu, kujifunza maandiko, sala, na imani ya kuamini. Aliwafundisha kwamba maamuzi madogo kwa muda husababisha maisha kamilifu, ya haki, na yenye furaha, na walifundisha mambo hayo kwa wengine. Ukiweka wote pamoja kuna zaidi ya watu 500 ambao wameingia Kanisani kwa sababu ya familia hii moja ya ajabu. Hii ni moja ya sababu nyingi kwa nini Bwana alinitaka kwenda kwenye misheni. Ilinifundisha matokeo ya milele ya kutafuta mapenzi ya bwana.

Yote ilianza na mazungumzo rahisi wakati wa chakula cha mchana. Mara nyingi mimi hufukiria kwamba ikiwa Dkt. Pingree angeshughulika zaidi na kazi yake ama mambo mengine ya kidunia, hangewahi kuuliza ni kwa nini sikuwa ninahudumu misheni. Lakini lengo lake lilikuwa kwa wengine na kwa kuendeleza kazi ya Bwana. Alipanda mbegu ambayo imemea na imezaa matunda na inaendelea kukua zaidi, kuongezeka kipeo. Mawazo yenye maongozi hutoa vitendo vizuri; vitendo vizuri hutoa vitendo vingine vizuri, na kuendelea, milele.

(Marko 4:20). Inasema, “Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia”

Wazo kwamba vitendo vidogo, rahisi lakini vilivyokusudiwa vinaweza kuwa na matokeo makuu limeungwa mkono vyema katika maandiko. Alma alimfundisha mwanawe Helamani:

“Kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka.  …

“… Kwa njia ndogo sana Bwana hufawadhaisha wale werevu na kutimiza wokovu war oho nyingi” (Alma 37:6–7).

Mojawapo wa somo la maisha la mwanzoni inapaswa kuwa kwamba kuna nguvu kuu katika athari ya ukuzwaji wa vitu vidogo ambavyo tunavifanya kila siku. Vitu vidogo na rahisi vinafanya kazi katika maisha yako hivi sasa---vikifanya kazi nawe ama kinyume nawe. Kama tu vile Bwana anavyotumia vitu kama hivi kukujenga, Shetani anavitumia kukuongoza na kukuelekeza pole pole, karibu bila kuonekana, kutoka kwenye njia.

Changamoto yetu ni kwamba tunapoona familia nzuri ama mtu aliyeifanikiwa kifedha ama mwenye kipaji kikubwa kiroho, hatuoni vitendo vyote vidogo na rahisi vinavyowatengeneza wao. Tunatazama wanariadha wa Olimpiki, lakini hatuoni miaka ya mazoezi ya kila siku iliyowafanya wawe mabingwa. Sisi huenda dukani na kununua matunda mazuri, lakini hatuoni kupandwa kwa mbegu na ukuzaji kwa makini na kuvuna. Tunamtazama Rais Monson na Wakuu Wenye Mamlaka wengine, na tunahisi nguvu na uzuri wao wa kiroho, lakini kile ambacho hatuoni ni vitendo vile rahisi vya nidhamu vya kila siku vikirudiwa kila mara. Vitu hivi ni rahisi kufanya, lakini ni rahisi pia kufanya---hususani kwa sababu matokeo si ya mara moja.

Tunaishi katika dunia ambao mambo mengi ni ya mara moja. Tunataka kwenda moja kwa moja kutoka kupanda hadi kuvuna. Tumezoea sana kupata matokeo ya mara moja---wakati wowote tunalazimika kungoja zaidi ya sekunde chache ili google ijibu maswali yetu yote, tunachukizwa---lakini tunasahau kwamba matokeo haya ni jitihada zilizokusanywa na vizazi vya kazi na dhabihu.

Alma anampa Helamani ushauri ambao ni mzuri sana kwetu leo. Akizungumzia Liahona na “miujiza mingine mingi” iliyoongoza familia ya Lehi “siku hadi siku,” alisema:

“Kwa sababu hiyo miujiza ilitendeka kupitia kwa njia rahisi iliwaonyesha kazi za kushangaza. Walikuwa wavivu na walisahau kutumia imani yao na bidii na baadaye zile kazi za ajabu zilikoma, na hawakuendelea kwenye safari yao.  …

“Ee mwana wangu, usituache tuwe wavivu kwa sababu ya urahisi wa njia; kwani hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa baba zetu; kwani hivyo ndivyo ilivyotayarishwa kwa ajili yao, kwamba ikiwa wangeangalia wangeishi; hata hivyo iko pamoja nasi. Njia imetayarishwa, na ikiwa tutaangalia tutaishi milele.

“Na sasa, mwana wangu, ona kwamba unalinda vitu hivi vitakatifu, ndio, ona kwamba umeelekeza jicho kwa Mungu na uishi.” (Alma 37:40–41, 46–47).

Vitu Vitatu Vidogo na Rahisi

Ninataka kuzingatia njia tatu ndogo na rahisi “kuelekeza macho yetu kwa Mungu” ambazo zitatusaidia kudumisha msisitiozo wetu wa kusudi wa milele. Hakuna kati yao itakayewashangaza---mmesikia mara nyingi awali. Lakini ninashuhudia kwamba kufanya vitu hivi kila mara na kwa kusudi halisi hakufanyi tofauti tu, kunafanya tofauti yote. Kama mnaelewa---ninamaanisha kuelewa kwa kina-kwa nini nyuma ya nidhamu hizi rahisi, bila maswali, mtazifanya kipau mbele cha juu katika maisha yenu.

Kwanza, tunapokea sakramenti, mara nyingi sisi hupitia vitendo tu. Mnapotazama video hii, tambua msisitizo iliyowekwa kwenye kukumbuka, na fikiria ni kwa nini jambo hilo ni muhimu sana.

Mzee Jeffrey R. Holland: “Pasaka ya mwisho na iliyoandaliwa kwa njia ya kipekee ilipokuwa inaisha, Yesu alichukua mkate, akashukuru, na akaumega, na kuwapa Mitume wake, akisema:”

Yesu Kristo: “Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.”

Mzee Holland: “Tangu tukio hilo la chumba cha juu la mkesa wa Gethsemane na Golgotha, watoto wa ahadi wamekuwa katika agano kukumbuka dhabihu ya Kristo kwa njia hii mpya, kuu, takatifu zaidi, na ya kibinafsi. Na kikombe kidogo cha maji tunakumbuka kumwagika kwa damu ya Kristo na kina cha mateso yake ya kiroho.

“Na gamba la mkate, daima likiwa limemegwa, limebarikiwa, na kutolewa kwanza, tunakumbuka mwili wake uliopigwa na moyo uliovunjika.

“Katika lugha rahisi na nzuri ya sala za sakramenti makuhani vijana wanatoa, neno la msingi tunalolisikia linaonekana kuwa kumbuka.

“Ikiwa kukumbuka ndio juhudi ya msingi iliyombele yetu, ni nini kinachoweza kuja akilini mwetu wakati nembo hizo safi na za thamani zinatolewa kwetu?”

Yesu Kristo: “Na hii mtafanya na itakuwa ushuhuda kwa Baba kwamba daima mnanikumbuka. Na ikiwa mtanikumbuka daima Roho yangu itakuwa na ninyi.”

Maandishi kwenye skrini: Je, “Utamkumbukaje daima?” 5

Tunapomkumbuka daima na kutii amri Zake, fikiria jinsi athari iliyojumuishwa ya kuwa na Roho Mtakatifu daima nasi huenda ikaadhiri kila sehemu ya maisha yetu. Fikiria jinsi ingeshawishi maamuzi yetu ya kila siku na ufahamu wetu wa mahitaji ya wengine.

Kuna njia nyingi sana tunaweza kutunza ahadi yetu ya kumkumbuka daima Mwokozi katika siku. Jinsi gani utamkumbuka daima?

Wengi watasema, “Sali na ujifunze maandiko.” Na mtakuwa sawa, kama, na hiyo ni kubwakama , itafanywa kwa kusudi halisi.

Kusali na kujifunza maandiko ni vitu viwili vinavyofuata vidogo na rahisi ambavyo ningependa kuhimiza.

Bwana yuko wazi kuhusu jinsi sala zetu hazina athari tunapozitoa kutokana na mazoea: “Inahesabiwa ni uovu kwa mtu, kama ataomba na bila kuwa na nia kamili ya moyo; ndio, na haimfaidi chochote, kwani Mungu hampokei yeyote wa aina hii” (Moroni 7:9).

Kusudi halisi ya sala ni kufungua njia mbili za mawasiliano na Baba yetu wa Mbinguni, kwa nia ya kufuata ushauri wowote atakooutoa Yeye. “Shauriana na Bwana kwenye matendo yako yote, na atakuongoza kwa yale mema; ndio, unapolala usiku lala katika Bwana, ili akulinde usingizini mwako; na unapoamka asubuhi hebu moyo wako ujazwe na shukrani kwa Mungu; na ukifanya vitu hivi, utainuliwa katika siku ya mwisho” (Alma 37:37).

Sala na kujifunza maandiko kwa asili huenda pamoja. Tunapojifunza maandiko na maneno ya manabii wetu wa sasa huandaa pampu ya ufunuo wa kibinafsi. Mifano na tahadhari zinazopatikana katika maandiko hufundisha hamu zetu. Hivi ndivyo tunavyokua ili kujua akili na mapenzi ya Bwana.

Manabii wa kale na sasa wametusihi tufanye vitu vidogo na rahisi kama kusali na kujifunza maandiko. Basi kwa nini kila mmoja wetu hafanyi hivyo ? Pengine sababu moja ni kwamba hatuoni hasa matokeo hasi kama tukikosa siku moja ama mbili---kama tu vile meno yako yote hayaozi yote na kuanguka mara ya kwanza unaposahau kupiga mswaki. Matokeo mengi, chanya na hasi, yatakuja baadaye, baada ya muda. Lakini yatakuja.

Miaka mingi iliyopita nilipanda miti miwili ya aina moja na urefu sawa katika kipande cha ardhi nyuma ya nyumba yangu. Nilipanda moja ambapo ulipata jua kidogo kila siku, na nilipanda mwingine ambapo ulipata jua kamili. Baada ya mwaka sikutambua tofauti kubwa katika kukua kwa miti ile miwili, lakini kisha mke wangu na mimi tulienda kwa misheni ya miaka mitatu. Tuliporudi, nilishangazwa na tofauti mkubwa! Athari ya jumla ya jua zaidi kiasi kila siku ilifanya tofauti mkubwa---baada ya muda---katika ukuaji wa miti ile. Jambo sawa na hilo hutendeka katika maisha yetu tunapojifunua kila siku kwa chanzo cha mwangaza wote. Huenda tusigundue mabadiliko ya mara moja, lakini muwe na uhakika kwamba mabadiliko yanatokea ndani yako, na matokeo yataonekana katika muda.

Wazo hili rahisi la athari ya jumla ya nidhamu ya kila siku, na kusudi na nia kamili, linaweza kuleta tofauti makubwa katika sehemu zote za maisha yako. Linaweza kumaanisha tofauti kati ya kung’ang’ana kupitia maisha ya kawaida ama kuwa na mafanikio makubwa na kukamilisha kipimo cha kuumbwa kwako.

Mara nyingi nimewazia maisha yangu na kustaajabu kwa nini ilikuwa ni vingumu mno kwangu kufanya uamuzi wa kwenda misheni. Ilikuwa ngumu kwa sababu nilipoteza mtazamo wa kusudi langu la milele. Tamaa zangu na mapenzi yangu hayakuwa sambamba na mapenzi ya Bwana; la sivyo, uamuzi ungekuwa rahisi sana. Na kwa nini hayakuwa sambamba? Nilienda kanisani na kushiriki sakramenti Jumapili---lakini bila kusudi halisi. Nilisali, lakini mara nyingi nilikuwa ninatenda tu. Nilisoma maandiko, lakini mara moja moja na bila kusudi halisi.

Kama mlivyosikiliza leo, ninatumai mmehisi, kupitia minong‘ono ya Roho, kile mnapaswa mfanye ili kuishi maisha ya kimakusudi na yenye mwelekeo. Ninawahimiza mfuate misukumo hiyo. Msikatishwe tamaa na mawazo ya kile ambacho tayari mmefanya ama hamjafanya. Mwacheni Mwokozi awape mwanzo mpya. Kumbukeni kile Bwana amesema: “Mara walipotubu na kuomba msamaha, na kusudi halisi, walisamehewa” (Moroni 6:8; mkazo umeongezwa ).

Anza sasa. Ishi maisha yenye kusudi. Weka nguvu ya ujumuishaji wa nidhamu ya kila siku pafaapo katika sehemu muhimu ya maisha yako. Ninaahidi kwamba mwaka moja kutoka sasa aitha utakuwa na furaha ulianza leo ama utatamani ungeanza .

Ningependa mtafakari maswali haya matatu: Ninawaalika mshiriki majibu yenu kwenye mitandao ya kijamii kuwa kutumia #ldsdevo.

Kwanza Unaweza kufanya? Je inawezekana kwako kufanya vitu hivi vitatu vidogo na rahisi? Unaweza kujitahidi kuishi agano lako “daima kumkumbuka yeye” (M&M 20:77, 79)? Unaweza kuweka muda wa kusali kwa uaminifu na kujifunza maandiko kila siku?

Pili: Je,Itafanya kazi? Je, unaamini kweli ahadi ya Bwana? Je, unaamini kwamba athari iliyojumuishwa ya kuwa na Roho wake daima itakuwa na ushawishi mkuu kwenye vipengele vyote vya maisha yako?

Mwishowe: Je, ina thamani yoyote?

Ninashuhudia kwambani ya thamani na inafanya tofauti yote, Unapofanya mambo haya, utagundua kwamba “kwa nini” ya msingi nyuma ya kila kitu unachokifanya ni kwamba unampenda Bwana na kutambua Upendo wake mkuu kwako. Na kila mmoja wetu apate furaha katika utafutaji wenu wa ukamilifu na katika kuelewa na kufanya mapenzi Yake. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Leo Tolstoy, in Peter T. White, “The World of Tolstoy,” National Geographic, June 1986, 767, 790.

  2. Inahusihswa na Mark Twain.

  3. Tad R. Callister, “Our Identity and Our Destiny” (Brigham Young University Campus Education Week devotional, Aug. 14, 2012), 9; speeches.byu.edu.

  4. “Apology,” The Dialogues of Plato, trans. Benjamin Jowett, 38a.

  5. Imetoholewa kutoka kwa video ya Always Remember Him”; lds.org/media-library; see also Jeffrey R. Holland, “This Do in Remembrance of Me,” Ensign, Nov. 1995, 67–68.

Chapisha