Mikutano ya Ibada ya Ulimwenguni Kote
Kuonja Nuru


Kuonja Nuru

Jioni pamoja na Mzee LynnG. Robbins Ibada ya Ulimwenguni Kote kwa Vijana Wazima • Mei 3, 2015 • Salt Lake Tabernacle

Ndugu na akina dada, karibuni kwenye hii Ibada ya Ulimwenguni Kote kwa Vijana Wazima, pamoja na makaribisho ya kipekee kwa wale kati yenu ambao watahitimu mwaka huu kutoka seminari---mafanikio ya kusifika na ushahidi wa imani yenu na upendo wa Bwana. Ninawalikeni nyinyi kufuata mfano wa wengine wengi hapa usiku huu na mwendelee na kujifunza kiroho katika chuo cha dini cha kwenu au kwenye chuo kikuu cha Kanisa. Ninawaahidi kwamba mtaendelea kupokea mwongozo muhimu kwa ajili ya maamuzi mengine katika maisha yenu, vilevile kukutana na watu ambao watakuwa na matokeo yenye maana katika maisha yenu.

Usiku wa leo mtanisikia mimi nikitoa ushahidi wangu wa Bwana Yesu Kristo na injili Yake. Mtanisikia mimi nikitumia maneno “Ninajua.” Ninataka kuwaelezeni jinsi nilivyo kuja kujua kwamba Yeye ni Mwana halisi wa Mungu, Mkombozi na Mwokozi wa Ulimwengu, na kwamba injili Yake ni ya kweli.

Pia ninataka kuwasaidieni mgundue kwamba ushuhuda wenu wenyewe wa Bwana Yesu Kristo na injili Yake ni mkubwa sana kuliko mnavyoweza kufikiria.

Uko Wapi Ushuhuda Wangu kwenye Spectra ya Imani?

Ningependa kuanza kwa nyinyi mkifanya tathmini binafsi ya kiakili. Tazameni mstari katika kielelezo hiki kisha mualamishe ushuhuda wenu kwenye hii spectra ya imani.

Chini kabisa ni mkanamungu.Tutampa mkanamungu alama ya sufuri. Juu katika mizani ni 10, au ni kuwa na ufahamu kamili wa Yesu Kristo na injili Yake. Wewe binafsi utajiweka wapi kwenye spectra hii? Ninadhani kwamba wengi wenu, mtajipa wenyewe alama ya chini kuliko mnavyostahili.

Kumbukeni alama mlizojipa wenyewe ili kuona kama inaongezeka wakati wa utoaji wa mada hii tunapojadiliana vipengele mbalimbali vya ujenzi wa imani wa ushuhuda na jinsi kila moja inavyosaidia kutuendeleza kwenye spectra ya imani na kutupa uzoefu mkubwa wa amani na furaha.

Alma anamwalika kila mtu kuchukua hatua ya kwanza mbele katika spectra ya imani kwa “majaribio juu ya maneno yangu na kutumia sehemu ya imani, ndio, hata kama hamuwezi tena kutamani kuamini” (Alma 32:27; msisitizo umeongezewa).

Tamani

Umaizi ufuatao unaelezea hekima ya kuchukua hatua hii ya kwanza ya kutamani.

Katika mwaka wa 1623 mtoto mwerevu sana wa Kifaransa, mwanahisabati, na mvumbuzi Blaise Pascal alizaliwa. Miongoni mwa uvumbuzi wake mwingine ulikuwa nadharia ya hisabati ya uelekeo, ambao ulitoa sayansi iliyo kiini cha uchaguzi wa nadharia ya kirazini---kukaribia kimaantiki kwa kufanya maamuzi ya bora zaidi. Pamoja na maamuzi ya nadharia, Pascal kwa werevu aliona kwamba katika mchezo wa maisha wanadamu hawawezi kukwepa dau kubwa sana la maisha: kuna Mungu ama hakuna. Imejulikana kama Dau la Pascal, kwa maisha ya mtu---au kwa uhalisia zaidi, maisha yao ya milele---kwa mambo kama yalivyofafanuliwa katika kielelezo hiki:

Katika vichwa vya safu vya habari zipo chaguzi mbili; Mungu yupo au hayupo. Katika mistari pia kuna chaguzi mbili: Ninaweza kuchagua kuamini au kutokuamini.

Michanganyiko inayoweza kutokea ni kama ifuatavyo:

  • Kama Mungu yupo na ninaamini na kufanya vilivyo, ninaweza kurithi uzima wa milele.

  • Kama ninaamini na Mungu hayupo, sipotezi chochote.

  • Kama siamini wala kuheshimu au kumtii Mungu na Yeye yupo, ninapoteza uzima wa milele.

  • Kama siamini na Mungu hayupo, sipati chochote.

  • Dau la Pascal linahoji kwamba uamuzi wa kweli ni kuamini katika uwepo wa Mungu na, kwamba ni mtu mjinga tu angepinga dhidi ya uwepo wa Mungu kwa sababu ana kila kitu cha kupoteza na hana chochote cha kupata.

Mwana mpotevu angebisha kwamba kile anachopoteza ni nafasi ya “kula, kunywa, na kufurahi” (2 Nefi 28:7)—faraja ya zawadi hafifu unapofikiria kile kilichopo hatarini. Anaweza “kuwa na furaha katika kazi (zake) kwa kipindi, [lakini] baadae mwisho unakuja” (3 Nefi 27:11). Ndoto zake za kufanya furaha na kufurahia zinakuwa jinamizi liishilo wakati anapotarajia kuamka kwenye kasumba ya kiroho aliyozoea katika maisha yake na anagundua yeye mwenyewe kwamba “uovu kamwe haujapata kuwa furaha” (Alma 41:10) na baadaye, siku ya hukumu, wakati “atakapotubu mbele ya Mungu kwamba hukumu zake ni za haki” (Mosia 16:1). Katika wakati wake anajifunza kwamba amedanganywa na bwana stadi wa uongo kwa anasa iliyopakwa sukari ya huzuni uliojificha. Kwa hiyo, “usiuache moyo wako uwaonee wivu wenye dhambi” (Mithali 23:17).

Tunashukuru kwamba kulikuwa na nafasi ya pili kwa mwana mpotevu, mojawapo ya masomo makuu Mwokozi anatutegemea sisi kujifunza kutoka fumbo hili (ona Luka 15:11–32).

Panda Mbegu---Anza Kujifunza

Alma anaelezea hatua inayofuata:

“Acha tamaa hii ifanye kazi ndani yako, hata mpaka utakapo amini katika njia ambayo unaweza kutoa nafasi kwa sehemu ya maneno yangu.

“Sasa, tutalinganisha neno kwa mbegu. Sasa, ikiwa utatoa nafasi, [uache] mbegu … ipandwe katika moyo wako” (Alma 32:27–28; msisitizo umeongezewa).

Kupanda mbegu humaanisha sasa umetenda juu ya tamaa pamoja na upekuzi wa kuvutia katika jaribio. Sasa umeanzisha njia ya kujifunza.

Kulingana na maandiko, njia hii ya kujifunza inatakiwa iendelee katika njia mbili: “Na kwa vile wote hamna imani, tafuteni kwa bidii na kufundishana maneno ya hekima; ndiyo, tafuteni kutoka kwenye vitabu vizuri maneno ya hekima; tafuteni maarifa, hata kwa kujifunza na pia kwa imani” (M&M 88:118; msisitizo umeongezewa).

Maandiko pia yanatufundisha juu ya njia mbili za kujifunza ambazo Roho anatufundisha:

“Ndiyo, tazama, Nitakuambia katika akili zako na katika moyo wako, kupitia Roho Mtakatifu, ambaye atakuja juu yako na ambaye atakaa ndani ya moyo wako.

“Sasa, tazama, hii ndiyo roho ya ufunuo” (M&M 8:2–3; msisitizo umeongezwa).

Kupanga Taratibu za Kujifunza na Njia za Kujifunza

Kabla ya kurudi kwenye spectra ya imani, ninataka nitoe kielelezo cha uhusiano kati ya taratibu mbili za kujifunza na njia mbili za kujifunza. Ukiziunganisha kwa kupitana zitakupa baadhi ya utambuzi wenye msaada juu ya jinsi tunaweza kusonga mbele katika spectra ya imani.

Wakati Joseph Smith alipojifunza kuhusu sala kwa kujifunza, alikuwa anasoma katika Biblia, “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa” (Yakobo 1:5).

Joseph alijifunza kuhusu sala kwa imani wakati alipofanya kwa imani yake na kwenda katika Kichaka Kitakatifu na akasali.

Juu ya kielelezo zipo njia mbili za kujifunza---akili na moyo.

Kuunganisha Maarifa kwa Kujifunza kwa Akili

Tunapotafuta maarifa kwa kusoma, Bwana anasema kwenye akili zetu katika umbo la mawazo yanayovutia. Miongoni mwa maneno mengine yanayowezekana kuhusiana na makutano ya “Kusoma” na “Akili,” tungeweza kuongeza yafuatayo: mawazo, upendeleo, udadisi, ukaguzi, kujifunza, kupekua, kuangalia, maswali, na kutafakari.

Maswali ya kuvutia yanasababisha mtu kutafakari, na kutafakari chini ya ushawishi wa Roho inayokuchukua wewe kwenye kiwango kifuatacho cha kujifunza, ambapo kusoma kunakingamana kwa moyo.

Kuunganisha Maarifa kwa Kujifunza kwa Moyo

Kutafakari kwako kunarutubisha mbegu, na inaanza kuota, na unaanza kuwa na hisia zilizovutia kupitia kwa Roho. Ni moyo, au hisia zilizovutia, ambazo zinabadili wazo kuwa imani.

Alma anaelezea kwa njia hii: “Ikiwa itakuwa mbegu ya kweli, au mbegu mzuri, ikiwa hamtaitupa nje kwa kutoamini kwenu, kwamba mtashindana na Roho wa Bwana, tazama itaaanza kuvimba ndani ya vifua vyenu, na wakati  mtasikia huu mwendo wa kuvimba, mtaanza kusema ndani yenu---inawezekana kwamba hii ni mbegu nzuri, au kwamba neno ni zuri, kwani linaanza kukua ndani ya nafsi yangu; ndio, inaanza kuangaza kuelewa kwangu, ndio, inaanza kunipendeza mimi” (Alma 32:28; msisitizo umeongezwa).

Huku kwa kawaida tunahusisha neno kusikia na akili, mara nyingi maandiko yanahusisha uelewa na moyo, kama vile; “Na mioyo yao ilifunguka na walisikia katika mioyo yao maneno ambayo aliomba” (3 Nefi 19:33). Wakati alipozungumza kuhusu Yakobo 1:5, kijana Joseph alisema, “Kamwe kifungu chochote cha maandiko hakijawahi kumwingia mtu moyoni kwa nguvu nyingi kuliko hiki kilivyofanya wakati huu” (Joseph Smith—Historia 1:12).

Pamoja na aina hiyo ya hisia, Alma anasema, “Sasa tazama, si hii itaongeza imani yenu? Ninawaambia, Ndio; walakini haijakuwa kwa ufahamu kamili” (Alma 32:29; msisitizo umeongezwa)

Haijawa bado uelewa kamili. Hata hivyo, pamoja na moyo ulioguswa, inatuvutia sisi kuchukua hatua nyingine kwenye spectra ya imani. Kwa Joseph, ilimvutia kutenda na kukubali mwaliko wa kimaandiko kuomba. Asingeweza “kupata ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani [yake]” (Etheri 12:6).

Kuunganisha Maarifa kwa Imani na Akili

Kujifunza kwa imani kunahitaji kutenda kwa hisia na imani.1 Mwokozi alitoa mwaliko huu wa kweli kujifunza kwa imani wakati aliposema, “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu” (Yohana 7:17; msisitizo umeongezwa). Katika aya hii Mwokozi anatufundisha kwamba kufanya ni tendo la imani ambalo linageuza imani kuwa maarifa, “Kwa wasemaji wasiokubali Anasihi, “Ijapokuwa hamniamini mimi, ziamini zile kazi: mpate kujua, na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, na mimi ndani yake (Yohana 10:38; msisitizo umeongezewa).

Katika kuzungumzia kujua, Alma anasema:

Na sasa, tazama, kwa sababu mmejaribu utafiti, na kupanda mbegu, na inavimba na kumea, na kuanza kukua, ni lazima mjue kwamba mbegu ni mzuri.

“Na sasa, tazama, ufahamu wenu ni kamili? Ndio, ufahamu wenu ni kamili kwa kile kitu, na imani yenu inalala; na hii kwa sababu mnajua, … ufahamu wenu umeanza kuelimika, na akili zenu zinaanza kupamuka” (Alma 32:33–34; msisitizo umeongezwa).

Kutenda kutokana na imani zenu kumewapeni elimu.

Miongoni mwa maneno mengine tunayoweza kuhusisha na kujifunza kwa imani na akili, tunaweza kujumuisha yafuatayo:

Alma anatumia kitenzi onja katika njia ya kipekee sana anaporejelea kuonja nuru. Sikiliza:

“Ee basi, si hii ni kweli? Nawaambia, Ndio, kwa sababu ni nuru: na chochote ambacho ni nuru, ni kizuri, kwa sababu kinaonekana, kwa hiyo lazima kwamba ni kizuri; na sasa tazama, baada ya nyinyi kuonja nuru hii si ufahamu wenu ni kamili?

“Tazama nawaambia, hapana, wala msiweke kando imani yenu, kwani mmejaridu tu imani yenu kupanda mbegu kwamba mngejaribu utafiti kujua kama mbegu ilikuwa mzuri (Alma 32:35–36; msisitizo umeongezwa).

Ni kwa kuonja nuru na kuifurahia ndiko kunakokupa elimu kamili katika kitu kile, au kujua kwamba mche ni mzuri. Nuru inawaalika nyinyi kuja kwa Yesu Kristo, “na uwezo wa Mungu [ukifanya] miujiza ndani [yenu] … na [kuwabadilisha nyinyi] kwenda kwa Bwana” (Alma 23:6).

Kuunganisha Maarifa kwa Imani na Moyo

Alma anaendelea; “Na tazama, wakati mti unaanza kukua, mtasema: Na tuurutubishe kwa uangalifu mkubwa, … kwa bidii kubwa, na pamoja na uvumilivu, mkitazamia tunda lake. …

“… Tazama, baadaye mtachuma [au kuonja] tunda hilo ambalo, ni la dhamani sana” (Alma 32:37, 41–42; msisitizo umeongezwa).

Kuonja tunda kunatupeleka mbele kwenye kujifunza kwa imani na kwa moyo hukutana. Hapa tunagundua sisi wenyewe kwamba tunda ni kwa kweli tamu na ni la thamani kuu, kumfuata Yesu Kristo, na kufanya kazi Yake, kunaturuhusu sisi kuonja upatanisho Wake na injili katika njia nyingi. Mwanzo katika njia mioyo yetu ilikuwa imeguswa kwa kina. Sasa “badiliko kuu likafanyika katika moyo” linatokea, kama lilivyoelezwa na Alma (Alma 5:12), na Roho anageuza uzoefu wetu na ufahamu kwenye mabadiliko.

Wakati tunapokuwa “tumemgeukia Bwana” (Alma 23:8), tunamfuata Mwokozi kwa kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Wakati “tunapoonja matunda” ya injili, tunapata uzoefu wa baraka; na shangwe na furaha mno kiasi kwamba tunataka kuwashirikisha wengine, kama Lehi alivyofanya: “Na nilipokula tunda lile lilijaza nafsi yangu na shangwe tele; kwa hiyo, nikaanza kutaka jamii yangu na wao pia wale; kwani nilijua kwamba lilikuwa tunda la kupendeza zaidi ya yote” (1 Nefi 8:12).

“Kumgeukia Bwana,”katika maana halisi, mabadiliko makubwa na mageuzi ya kuwa kama Yesu Kristo, kwa “[kukubali] ushawishi wa Roho Mtakatifu, na [kumvua] mtu wa asili na [kuwa] mtakatifu kupitia upatanisho wa Kristo aliye Bwana” (Mosia 3:19). Katika mambo mengi ya kweli ya neno, mabadiliko yetu hayawezi kukamilika mpaka tumekua kiroho “hata kufikia kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo” (Waefeso 4:13). Huu utakuwa ufuatiliaji wa maisha na safari ya imani katika Yeye na pamoja na neema Yake au msaada wa kiungu (ona 2 Nefi 25:23).

Mabadiliko haya ya maisha yote yatahitaji kwa udhahiri urutubishaji endelevu kwa upande wetu kuepuka hali ya kunyauka iliyoelezwa na Alma: “Lakini mkiuachia mti ule, na msifikirie kuurutubisha, tazama hautapata mzizi wowote; na wakati joto la jua linawadia na kuuchoma, … Hukaukia mbali”(Alma 32:38).

“Kwa hiyo, lazima msonge mbele mkiwa na imani katika Kristo, mkiwa mg’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo wa Mungu na Wanadamu wote. Kwa hiyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherehekea neno la Kristo, na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele” (2 Nefi 31:20; msisitizo umeongezwa).

Mabadiliko haya makubwa na uongofu hayamaanishi bado hatutakuwa na maswali. Badala yake, baada ya kuonja nuru, maswali bado yataweka ndani yetu tamaa ya kuendelea kujifunza badala ya kusababisha wasiwasi ambao unaweza kusababisha kunyauka kwa imani yetu inayokua. “Na yeyote atakayeamini katika jina langu, bila kuwa na shaka, kwake nitamhakikishia maneno yangu yote” (Mormoni 9:25).

Maswali ni mazuri. Yanatusababisha kutafakari, kutafuta, na kusali. Joseph Smith aliendelea kuwa na maswali katika maisha yake yote. Karibu kila sehemu ya Mafundisho na Maagano ilionyeshwa kupitia kwake kama matokeo ya maswali aliyoyapeleka kwa Bwana katika sala, mstari kwa mstari, na agizo kwa agizo. Hii ni njia ileile Mwokozi pia alijifunza: “Naye hakupokea utimilifu mwanzoni, bali aliendelea kutoka neema hadi neema, mpaka akapokea utimilifu” (M&M 93:13).

Ufahamu Kamili

Tukirudi kwenye spectra ya imani yetu, tuliweka kitambulisho kulia kabisa “ufahamu kamili wa Yesu Kristo na injili Yake.”

Acha tuchunguze kishazi “ufahamu kamili.” Katika kuhusisha “kuonja nuru,” Alma alifundisha kwamba “ufamamu wenu ni kamili kwa kile kitu” (Alma 32:34). Katika mstari ufuatao, tafuta matumizi ya nabii Mormoni ya msemo huo huo, “ufahamu kamili,” anapoongeza ushahidi wake wa nuru hiyo hiyo:

“Na tazameni, ndugu zangu, mmepewa nyinyi kuhukumu, ili muweze kujua mema na maovu; na njia ya kuhukumu ni dhahiri, ili muweze kujua kwa ufahamu kamili, kama mwangaza wa mchana ulivyo kutoka giza la usiku.

“Kwani tazama, Roho ya Kristo imetolewa kwa kila mtu, ili ajue mema na maovu; kwa hivyo, ninawaonyesha njia ya kuhukumu; kwani kila kitu kinachokaribisha kufanya mema, na kushawishi kuamini katika Kristo, kinasababisha na uwezo na thawabu ya Kristo; Kwa hivyo mgejua na ufahamu kamili kwamba ni cha Mungu. . …

“Na sasa, ndugu zangu, nikiona kwamba mnajua nuru ambayo kwake mnaweza kuhukumu, nuru ambayo ni nuru ya Kristo, mhakikishe kwamba hamhukumu kwa makosa” (Moroni 7:15–16, 18; msisitizo umeongezwa).

Manabii wote wawili wanashuhudia kwamba ni nuru ya Kristo ambayo inayotupa ufahami kamili wa ukweli. Hata watu wa ulimwengu wanatambua kwamba wana hisia za ndani za mema na mabaya. Ufahamu wao wa Nuru ya Kristo katika matumizi ya neno dhamiri, ambalo linatoka kutoka Kilatini neno conscientia, au “ufahamu ndani yako binafsi.”2

Pamoja na ile nuru kama alama ya ukweli, tunaendelea kusonga mbele kwenye spectra ya imani mstari juu ya mstari, na amri juu ya amri (ona 2 Nefi 28:30; M&M 98:12;128:21), “na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu mtajua ukweli wa vitu vyote” (Moroni 10:5; msisitizo umeongezwa).

Katika muda mfupi kwa kweli tutajaribu jaribio la Alma ili kwamba muweze kukumbushwa nuru ina ladha gani na jinsi inavyotupa ufahamu kamili.

Upinzani Hufunua Ukweli

Kabla ya kwenda mbele na jaribio, ni muhimu kutambua kipengele kingine cha muhimu katika njia. Tunafundishwa katika 2 Nefi 2 kwamba kuna “lazima kuwe na … upinzani katika vitu vyote” (2 Nefi 2:11). Wanadamu “waonje uchungu, ili waweze kujua kutunza chema” (Musa 6:55). Afya, kwa mfano, kimsingi ni mafunzo ya kinyume chake, ugonjwa; na maradhi; uhuru, somo la ukandamizaji na utumwa; furaha, somo la huzuni; na alkadhalika. Na kama muujiza mdogo wa kimulimuli, nuru inakwenda bila kuthaminiwa bila giza kwenye pazia la nyuma.

Upinzani ni lazima kwa elimu yetu na furaha. Bila huo, ukweli unabaki umefichika katika mwonekano wa wazi, kama kupuuza hewa mpaka wakati unapoipapia kwa nguvu. Kwa sababu Nuru ya Kristo iko wakati wote, watu wengi hawatambui Roho katika maisha yao, kama hao Walamani katika 3 Nefi 9:20 ambao “walibatizwa kwa moto na Roho Mtakatifu, na hawakujua.”

Upinzani haufunui tu au kufichua ukweli lakini unadhihirisha uwezo wake wa asili, furaha, na utamu. Kwa mfano, ilichukuwa ladha ya maisha machungu kwa mwana mpotevu kuelewa ni maisha gani matamu aliyoyaacha nyuma nyumbani na aliyokuwa amechukulia kama kawaida katika ujana wake.

Ni kupitia maumivu tu na ugonjwa ndipo tunakuja kudhamini afya zetu. Kama wahanga wa udanganyifu, tunauthamini uadilifu. Tukipata uzoefu wa udhalimu au ukatili, tunatunza upendo na wema---vyote kwa “ufahamu kamili,” tukiwa tumeonja tunda la kila mmoja na nuru ambayo ipo ndani yetu. Ufahamu kamili unakuja tunda juu ya tunda, kupitia upinzani katika vitu vyote. Utii kwa amri za Mungu unaahidi furaha mwishoni, ukuaji, na njia kupitia upinzani, sio kuukwepa. “Bahari zilizoshwari hazitengenezi mabaharia mahiri.”3

Fikiria kauli hii yenye umaizi kutoka kwa Nabii Joseph Smith: “Kwa kutoa uhasama, ukweli unawekwa wazi.”4

Na kutoka kwa Brigham Young: “Ukweli wote unathibitishwa na kuwekwa wazi kwa upinzani wake.”5

Jaribio la Imani

Sasa---acha nawe uwe mshiriki katika jaribio kwa kukufanya ufikirie baadhi ya amri za “kuwa” au uadilifu kama wa Kristo, ukitofautiana na kila moja wapo na kinyume chake. Unapofikiria kila moja, nuru ya Kristo ndani yako inapaswa ithibitishe kwenye akili zako na moyo kwamba kila moja ya uadilifu kama wa Kristo ni mtamu, wakati kinyume chake ni mchungu:

  • Upendo dhidi ya chuki, uadui, upinzani

  • Uaminifu dhidi ya uongo, udanganyifu, wizi

  • Kusamehe dhidi ya kisasi, chuki, uchungu

  • Upole dhidi ya uchoyo, hasira, ukatili

  • Uvumilivu dhidi ya hasira, ukaidi, kutovumilia

  • Unyenyekevu dhidi ya kiburi, kutofundishika, ufedhuli

  • Msuluhishi dhidi ya mbishi, mtenganishi, mchokozi

  • Bidii dhidi ya kuchoka, kata tamaa, kaidi

Hizi ni idadi chache tuu ya uadilifu kama wa Kristo, lakini zinatosha kwa uwazi kuonyesha athari ya jaribio la mbegu.

Katika kutafakari orodha hii mnagundua kwamba mmekuja kujua uwezo, ukweli, na utamu wa kila maadili, moja baada ya jingine, kupitia maelfu ya “uzoefu ulio dhibitishwa,” kama Mzee Neal A. Maxwell alivyoyaita. Tunda zuri linakuja na ushahidi wake kamili wa asili na udhibitisho wa---ladha yake. Ushahidi ni katika kula, tunda kwa tunda na mstari juu ya mstari, kila moja kwa “ufahamu kamili.” Labda hicho ndicho Mtume Paulo alimaanisha aliposema, “Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema” (1 Wathesalonike 5:21; msisitizo umeongezwa). Kama mmeunganisha haya na maadili mengine katika maisha yenu, mmesonga mbele zaidi kwenye spekra ya imani zaidi ya mlivyofikiria mlikuwa.

Hata hivyo, hiki ndicho pekee naweza kuita ushuhuda wa terestia, au wa utukufu-wa-mwezi. Mtu mwema wa dini yoyote amwogopaye ana ushuhuda huu huu kwa sababu wao pia wana Nuru ya Kristo, ambayo Mormoni alizungumzia, na wamekubali sehemu ya injili Yake.

Jaribio la Imani—Ngazi Inayofuata

Ushuhuda wa selestia, au wa utukufu-wa-jua, unakuja wakati mtu anapotafuta “ukamilifu wa Baba” M&M 76:75–78; 93:19). Wakati mtu anapobatizwa na anastahili karama za Roho Mtakatifu, Yeye hupokea endaumenti kubwa ya Nuru ya Kristo, kama ilivvyoandikwa katika mstari katika hiki Kitabu cha Mormoni: “Ikiwa hili ndilo pendo la mioyo yenu, ni nini mnacho dhidi ya kubatizwa kwa jina la Bwana, … ili awateremshie Roho wake juu yenu zaidi” (Mosia 18:10, msisitizo umeongezwa).

Rais Dieter F. Uchtdorf alitufundisha kwamba tunakua katika nuru: “Tunaelekeza zaidi mioyo yetu na akili zetu kwa Mungu, ndivyo nuru ya mbinguni inavyotiririka juu ya nafsi zetu.”6

“Na yule ambaye huipokea nuru, na kukaa ndani ya Mungu, hupokea nuru zaidi; na nuru hiyo huzidi kung’ara hata mchana mkamilifu” (M&M 50:24).

Sihitaji kukueleza kwamba wingi zaidi wa nuru huongeza uwezo wa kuona---mnajua hivyo. Nabii Joseph Smith alisema, “Mtu anavyokaribia zaidi ukamilifu, mawazo yake huzidi kuwa maangavu, na furaha yake huwa kubwa.”7

Kwa nuru kuu ya kuwezesha kuona, na tuchukue jaribio kwenye kiwango cha selestia, na kutofautisha baadhi ya mafundisho ambayo ni ya kipekee kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho na yale yanayopatikana kwingine chini ya nuru hafifu:

  • Mungu ni Baba yetu, na tumeumbwa katika mfano Wake dhidi ya Yeye sio Baba yetu hasa, asiyeeleweka, asiyejulikana

  • Mpangilio wake pamoja na manabii na mitume dhidi ya utelekezaji wa mpangilio Wake iliotengenezwa.

  • Bwana ni Mungu wa utaratibu, akitawala kupitia hao wanaoshikilia funguo za ukuhani dhidi ya machafuko, sauti tofauti, “Roho za uongo” (M&M 50:2)

  • Mamlaka ya ukuhani na kuitwa na Mungu dhidi ya shahada katika teolojia; mtu aliyechaguliwa, mtu aliyeajiriwa au aliyejiteua.

  • Ibada na maagano dhidi ya kuishi maisha ya mazuri tu.

  • Umaasumu wa watoto dhidi ya ubatizo wa watoto wachanga.

  • Kitabu cha Mormoni, ushahidi wa pili dhidi ya Biblia, ushahidi pekee

  • Kazi ya Hekalu kwa wafu dhidi ya kuwasha mshumaa na kuwaombea walio kufa.

  • Ndoa na familia za milele dhidi ya mpaka kifo kitakapo tutenganisha

Inaelimisha kutenganisha ukweli na kinyume chake. Inasaidia kuonyesha uwazi, kilichofichwa kuwa bayana. Tunatambua kwamba tunafahamu mengi zaidi kuliko tulivyofikiria tulijua. Inatakiwa ituvutie kuendelea kutafuta kwa bidii katika nuru ya Kristo … utashikilia kila kitu kizuri” (Moroni 7:19).

“Wa Heri Wale Wasioona, Wakasadiki” (Yohana 20:29)

Sasa acha tuchunguze kipengele kingine kinachovutia cha imani na ushuhuda.

Tunaelewa kwamba “imani ya [kweli] lazima iwe kitovu chake ni Yesu Kristo ili kwamba iweze kumwongoza mtu kwenye wokovu. …

“[Hiki] kinajumuisha tumaini kwa mambo ambayo hayaonekani, bali ambayo ni kweli [Waebrania 11:1].”8

Si inastajabisha kwamba imani ya kweli katika Yesu Kristo ni “kuamini bila kuona” wakati ulimwengu unaamini kinyume chake, kwamba “kuona ni kuamini”?

Mtu wa asili anagundua ulimwengu kupitia hisia tano, akidai ishara kama udhibitisho. Na bado maandiko yamejaa mifano ya hao waliopokea ufunuo wa uwepo wa Mungu na uwezo kupitia hisia tano bila kupokea mabadiliko ya kudumu:

  • Lamani na Lemueli walimwona malaika (ona 1 Nefi 3:29). Walisikia sauti ya Bwana ambayo “iliwakemea zaidi” (1 Nefi 16:39). Walihisi uwezo wa Mungu wakati Nefi alipounyoosha mkono wake na “Bwana aliwashitua” (1 Nefi 17:54). Walionja na wakanusa: “Nitakifanya chakula chenu kiwe kitamu, hata hamtakipika” (1 Nefi 17:12). Licha ya madhihirisho mara nyingi kupitia kwa hisia zote tano, waliasi.

  • Wakati Musa alipowaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, wao walishuhudia mateso, nguzo za moto, kujigawa kwa Bahari ya Shamu, walionja mana---uzoefu kwa hisia zote tano. “Na japokuwa walikuwa wakiongozwa, Bwana Mungu wao, Mkombozi wao, akiwatangulia akiwaongoza mchana na kuwapa nuru usiku, na kufanyia yote yaliyompasa binadamu kupokea, waliposhupaza mioyo yao na kupofusha mawazo yao, na kumtusi Musa pamoja na Mungu anaeishi na wa kweli” (1 Nefi17:30). Kuona kwa kweli hakukuwa kuamini kwa wao!

  • Kuna mifano mingine mingi kama hii katika maandiko, bali mifano yote mingi yenye bumbuwazi ni wasiokomaa kiroho ambao walimkataa Mwokozi mbele Yake kabisa. “Walakini japokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao hawakumwamini.” (Yohana 12:37; ona pia M&M 138:26)

Kuna mifano mingi sana iliyo kinyume na kusema kwamba kuona ni kuamini. Hao wanaotegemea kwa uzoefu wa kustaajabisha mmoja tu ili kusaidia kufafanua ushuhuda wao hawaelewi kwamba ushuhuda na ushahidi mkuu wa Roho unakuja kwetu kila siku, katika njia nyingi ndogo ndogo, kiasi kwamba mara ya mwisho ulipiga mstari chini ya maandiko yako. Fikiria kuhusu hilo. Sababu ya kupiga mstari chini ya maandiko yako ni kwa sababu ulipokea maono, utambuzi, “ile Ahaa!” ya utambuzi wa kuvutia ni ufunuo.

Mfano mwingine wa ufunuo ni wakati unaposhawishika kuwa mpole au kufanya jambo jema, “kwani kila kitu kinachokaribisha kufanya mema … kinasababishwa na uwezo na dhawabu ya Kristo” (Moroni 7:16). Nuru ya Kristo ipo wakati wote! Mnaionja kila siku. Na kutoka minong’ono hii, haya “mambo madogo[,] huja yale yaliyo makuu” (M&M 64:33).

“Kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu Mnaweza Kujua Ukweli wa Mambo Yote” (Moroni 10:5)

Unaweza kufikiri juu ya yoyote katika Kitabu cha Mormoni ambaye alimwona malaika na akaweza kuamini? Kuna uwezekano unamfikiria Alma kijana. Malaika alimtokea na wana wa Mosia na “Na alishuka kama kwa wingu; na alizungumza kwa sauti kama radi” (Mosia 27:11). Mnajua mwisho wa hadithi---Toba ya Alma na huduma yake baadaye.

Je! Kule kuona kulikuwa kuamini kwa Alma? La Hasha! Kwa nini? Kwa sababu Alma alikuwa bado hajatumia uhuru wake wa kuchagua katika kujifunza kwa kusoma na imani na alikuwa bado hajasali kujua ukweli. Kuona sio njia ya mkato kwenda kwenye imani au ushuhuda, kama ilivyoshuhudiwa katika mifano mingi iliyoonyeshwa hapo juu. Alma, mwenyewe anaelezea jinsi alivyopokea ushuhuda wake, na hakudhani hiyo ndiyo sababu ya kutokea kwa malaika. Kwa kweli, hakuna tamko la malaika popote kabisa katika ushuhuda wake:

“Na hii sio yote. Hamdhani kwamba ninajua vitu hivi mimi mwenyewe? Tazama, ninashuhudia kwenu kwamba ninajua kwamba mambo haya kwa hivyo niliyosema ni kweli. Na jinsi gani mnadhani kwamba ninajua uhakika wake?

“Tazama, ninawaambia kwamba yamesababishwa kujulikana kwangu na Roho Mtakatifu wa Mungu. Tazama, nimefunga na kusali siku nyingi ili nivijue vitu hivi mimi mwenyewe kuwa ni vya kweli, kwani Bwana Mungu amevudhihirisha kwangu kwa Roho wake Mtakatifu; na hii ni Roho ya ufunuo ambaye yuko ndani yangu” (Alma 5:45–46; msisitizo umeongezwa)

“Wito wa kuamsha” na mabadiliko ya muda mfupi katika tabia yanaweza kutokea kutoka nje kwenda ndani, kupitia hisia tano, lakini siku zote ni ya muda mfupi, kama kwa Lamani na Lemuel. Ushuhuda wa kuvumilia unaweza tu kuja kutoka ndani kwenda nje jinsi mtu anavyojifunza kwa kusoma na imani pamoja na Roho Mtakatifu akipanda injili “ndani yao, na katika mioyo yao [nitaandika]” (Yeremia 31:33). Hiyo ndiyo sababu Wanefi, ambao licha ya kuweza kuona, kusikia, na kumgusa Mwokozi wakati wa matembezi yake kwao,vilevile kuonja na kunusa mkate na divai iliyotolewa kimiujiza na Yeye (ona 3 Nefi 20:3–9), hata hivyo, [waliomba] wapate kile ambacho walitaka zaidi; na walitaka kwamba Roho Mtakatifu apewe kwao.” (3 Nefi 19:9).

Miaka michache iliyopita, hadithi ifuatayo ilishirikishwa kwangu na mmisionari mkubwa. Yalimtokea wakati alipokuwa kijana katika miaka ya 1960 na pia inaelezea kwa mfano kwamba ni kupitia tu kujifunza na sala ndipo Roho Mtakatifu anatupa ushahidi wa ukweli. Yeye alisema:

“Nilikuwa nakiishi peke yangu Provo, Utah, katika chumba kidogo cha kupanga karibu na katikati ya mji. Nilikuwa nikifanya kazi kama muuzaji katika duka dogo la fenicha katika Provo, na ilikuwa wakati wa wikiendi ndefu karibu na sikukuu ya mwaka mpya ndipo tukio hili lilitokea.

“Tulikuwa na sikukuu ndefu ya wikiendi. Ilikuwa Alhamisi, Disemba 31, Mkesha wa Mwaka Mpya. Tuliwa tumepewa ruhusa kazini kutoka Alhamisi mpaka Jumapili, na nilikuwa kwenye chumba changu bila mpango wowote wa kusherehekea. Nilikuwa ninatayarisha chakula changu cha usiku nikingojea kiive, na nilitaka kitu fulani cha kusoma. Kwa kutokuwa na chochote katika chumba, nilikwenda kwenye mlango wa pili kuwaomba vijana fulani waliokuwa wanaishi mle (wanafunzi wa BYU) kama walikuwa na chochote---nikitegemea nakala ya Field & Stream, au kitu fulani kama hicho, Walisema hawakuwa na magazeti yoyote lakini walikuwa na kitabu ningependa kukisoma. Walinipa nakala ya Kitabu cha Mormoni.

“Hali nilikuwa nimesikia kuhusu Kanisa la Mormoni (nani aliyepo Utah hajasikia?), Sikuwa na mazoea na kitabu hicho. Niliwashukuru na nilikichukua kitabu chumbani kwangu. Wakati nikila chakula cha usiku nilikipitia na nikaanza kukisoma. Ninakiri kwamba nilichunguza kupitia baadhi ya sehemu, nikijaribu kutafuta mtiririko wa hadithi. Kulikuwa na majina na maeneo kamwe sijawahi kuyasikia kabla, na sikuweza kuendelea. Kwa hiyo baada ya chakula, Nilikichukua kitabu hicho na kukirudisha pamoja na “hapana, asante sana”

‘“Je ulisali kukihusu?’ mmoja wa Vijana aliuliza. ‘Kusali kukikusu?’ Nilijibu. ‘Nilitaka tu kitu cha kusoma, siyo kitu nilitakiwa kusali kukihusu.’ Hii ilianzisha mazungumzo ya kufurahisha kuhusu yaliyomo katika Kitabu cha Mormoni. Waliniambia kwamba kilikuwa kitabu cha maandiko, kitabu ambacho kama kwanza ningesali na kisha kukisoma kwa tamaa halisi kujua kama kilikuwa cha kweli au la, kwamba Mungu angeonyesha ukweli wake kwangu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

“Nilikuwa nimelelewa kama Mkatoliki, na ingawa sikuwa mshiriki mkamilifu wakati ule, nilishikilia uumini wangu katika Kanisa Katoliki kwa kushikilia kwa nguvu kwa sababu lilikuwa ndilo nililolifahamu. Kusali pekee nilikowahi kufanya ilikuwa Sala ya Bwana, Salamu Maria, na kusoma katika misale yangu---kitu ambacho sijakifanya kwa muda mrefu sana. Na sasa vijana fulani walikuwa wananiambia nisali kwa Mungu sikuweza kwa hakika kuelewa na kumwomba Yeye anieleze kama kitabu kilikuwa cha kweli au la. Sawa, mambo gani haya, sikuwa na chochote zaidi cha kufanya, na ilikuwa wikiendi ndefu sana. Nilikichukua kitabu nyumbani, nikafungua chupa ya bia, nikawasha sigara, na nikapiga magoti na kumwomba Mungu aniambie kama kitabu hiki kilikuwa cha kweli. Kisha nikaanza kukisoma: ‘Mimi, Nefi, nikiwa nimezaliwa na wazazi wema.’

“Majina na maeneo yalikuwa sawa na yale niliyoyasoma masaa machache yaliyopita. Tofauti pekee wakati huu ilikuwa ni ‘kuondoshwa kwa kutoamini’ ambako kulikuja juu yangu kimiujiza. Nilikuwa kwa kweli katika kitabu! Niliweza kumwona Nefi; niliweza kuwaona kaka zake, na ilinikasirisha wakati walipomtesa. Nilimpenda Nefi! Niliwashangilia watu wazuri na niliwaonea huruma watu wabaya. Nilikisoma kwa masaa mengi, na sikuweza kukiweka chini kitabu hiki. Wakati mwishowe nilipoangalia saa, ilikuwa inakaribia saa kumi na moja za asubuhi. Nilijiambia mwenyewe Heri ya Mwaka Mpya na nikalala.

“Niliamka karibu saa mbili na nusu na bila kufikiri nikakichukuwa kitabu hiki. Na ndiyo njia wikiendi iliyobakia ilivyokwenda. Kama Kaka Parley P. Pratt, wazo la chakula lilikuwa la kipuuzi, sikutaka chochote kinisumbue. Nilizima simu yangu na nikasoma mchana kutwa, nikiwa na mkatizo mara chache wa vitafunwa. Kama usiku wa kwanza, ningeweza mwishowe kutambua ilikuwa mapema asubuhi, kulala masaa machache, kuchukua kitabu, na kuendelea marathoni yangu niliyojiwekea. Hatimaye, karibu saa kumi na moja siku ya Jumatatu asubuhi, nilimaliza kusoma kitabu na nikalala usingizi---nimechoka sana.

“Kabla ya Krismasi mwaka ule, nilikuwa nimeuza zulia kubwa eneo la American Fork. Lilikuwa ni aina maalum ya zulia, na bosi wangu alitaka mimi nisimamie matabaka ya zulia. Bosi wangu alikuwa askofu wa zamani katika eneo la Provo na alikuwa amenizungumzia kuhusu Kanisa nyakati mbalimbali, lakini sikuwa na habari nalo. Alikuwa Bosi mzuri, lakini usingependa umchokoze kwa sababu alikuwa na hasira. Ilikuwa asubuhi ya Jumatatu hii, saa mbili kamili, ambayo nilitakiwa kusimamia uwekaji wa zulia. Muda uliowekwa ukafika, na sikutokea; saa tatu kamili, kisha nne.

“Hatimaye, karibu saa 10:30, bosi wangu, kakasirika kama kuku aliyelowa, akaja kwenye chumba changu, akaingia ndani tayari kupasua kichwa changu, akaniona nimelala kwenye kochi na Kitabu cha Mormoni kipo kifuani pangu, na akabadilisha mawazo yake. Kimya kimya alifunga mlango na akarudi kwenye duka lake, akiwa na imani kwamba angeweza kuanza matabaka ya zulia. Mara baada ya saa tano na nusu niliamka (bila kujua juu ya matembezi ya bosi), niliangalia saa ya ukutani, na kwa mara ya pili kwa muda mfupi nikasali sala ingine. Nilivaa haraka (nikiamini kwamba wakati nitapofika kule labda sitakuwa na kazi iliyobaki), niliingia kwenye gari langu, nikaenda kwa haraka sehemu ya kazi.

“Nilimwona bosi wangu pale na nikamwendea kuomba radhi. Aligeuka; tabasamu likaja usoni mwake, na aliuliza, ‘Ulikionaje kitabu hicho?’ Nikielewa nini kilichotokea, mawazo yangu yalirudi nyuma kwenye wikiendi iliyopita, na kupitia macho yaliyojaa machozi nilisema jambo ningeweza kusema, ‘Kitabu ni cha kweli. Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu.’ Kisha nikaanza kulia, na alikuja na kunikumbatia na akanishika. Nilibatizwa kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho tarehe 22 Januari 1965.”

Nilikutana na kaka huyu mwema miongo kadhaa baada ya kuongoka kwake wakati akihudumia misheni pamoja na mkewe katika San Diego Mormon Battalion visitors’centre. Sababu naipenda hadithi hii sana ni tofauti katika kujaribu kwake mara mbili kusoma kitabu cha Mormoni. Mara ya kwanza alianza kusoma, ilikuwa bila nia ya kweli au sala. Katika jaribio la pili, kwa tamaa na sala, ilikuwa kabisa uzoefu tofauti.

Kuna njia moja tu ya kujua kama Kitabu cha Mormoni na injili ni ya kweli, na inachukua zaidi ya udadisi na zaidi ya hisia tano. Inachukua matumizi ya kweli ya uhuru wa mtu kujiamulia na kutenda juu ya tamaa ya kujua.

“Na mtakapopokea vitu hivi, ningewashauri kwamba mgemwuliza Mungu, Baba wa milele, katika jina la Kristo, ikiwa vitu hivi si vya kweli; na ikiwa mtauliza na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

“Na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu mtajua ukweli wa vitu vyote” (Moroni 10:4–5).

Ahadi ile sio ya kufundishwa katika maneno ya “Anaweza” au “pengine” au ‘labda.” Ahadi ni “Ataonyesha ukweli wake kwako, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.”

Kanuni nyingine ya uelewa tunoagundua katika hadithi hii ni kwamba hauna haja ya kusoma Kitabu cha Mormoni chote kabla ushahidi haujaja. Mtu katika hadithi hii, yeye alionja nuru kwenye ukurasa wa kwanza. Hakuhitaji kula pizza mzima kabla hajajua utamu wake. Kwa wengine, inaweza kuwa zaidi ya ladha ya kujizoesha wakati nuru inapokuwa tamu zaidi baada ya muda. Hiyo inaonekana kuwa kile Alma anachosema katika mstari huu: “Ndio, inaanza kuangaza kuelewa kwangu, ndio, inaanza kunipendeza mimi” (Alma 32:28).

Ushuhuda Wako Una Nguvu Zaidi Kuliko Unavyofikiria Ulivyo

Tulipokuwa tunaanza niliwaambieni mhesabu ushuhuda wenu juu ya spectra ya imani. Natumaini kwamba mmegundua kwamba ushuhuda wenu umeimarika zaidi ya vile mlivyofikiria. Kwa Roho Mtakatifu kama mwalimu wenu, mmekuwa mkiongeza ufahamu kamili wa matunda mengi ya injili, msitari juu ya msitari, ushuhuda wenu umekuwa unakomaa kila siku.

Zaidi mtu anavyojifunza na kuishi injili, ndivyo zaidi nuru wanayopokea na zaidi mpango wa Baba unakuwa injili ya maarifa ya kawaida. Tunajifunza kutoka uzoefu wetu wenyewe kwamba tunda la mti wa uzima, kwa kweli, ni la dhamani na “tamu mno, zaidi ya yale yote ambayo [sisi] tumewahi kuonja” na kwamba linajaza roho zetu “na shangwe tele” (1 Nefi 8:11–12). Tunaendelea kwa kulipenda kwa sababu ya baraka, furaha, na mamlaka ambayo linatupatia sisi juu ya matokeo chanya katika maisha yetu na matumaini ya furaha isiyo na mwisho kama familia milele.

Ninatoa ushahidi wangu kwamba ninajua, na ninajua kwamba ninajua, kupitia Roho Mtakatifu, kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu. Ni kitamu na ni chenye thamani kwa ladha. Nakipenda na kukihifadhi kwa upendo wa ladha yake. Ninatoa ushahidi kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na kwamba alisulubiwa na kuteseka kwa dhambi za ulimwengu. Ni Mwokozi wetu na anaendelea kuliongoza na kulisimamia Kanisa na ufalme Wake hapa duniani kupitia manabii na mitume waliohai. Ninatoa ushahidi wa jina Lake na ukweli huu katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona David A. Bednar, “Seek Learning By Faith,” Ensign, Sept. 2007, 60–68.

  2. OnaWordsense.eu Dictionary, “conscientia,” www.wordsense.eu/conscientia/.

  3. Mithali ya Kiafrika.

  4. Joseph Smith, katika Historia ya Kanisa, 6:428.

  5. Brigham Young, Discourses of Brigham Young, sel. John A. Widtsoe [1954], 433.

  6. Dieter F. Uchtdorf, “Receiving a Testimony of Light and Truth,” Ensign auLiahona, Nov. 2014, 22.

  7. Joseph Smith, katika Historia ya Kanisa, 2:8.

  8. Guide to the Scriptures, “Faith,” scriptures.lds.org.

Chapisha