“Jina la Kanisa Lake,” Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Okt. 2021.
Ujumbe wa Kila Mwezi wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana Oktoba 2021
Jina la Kanisa Lake
Kuna maana katika jina ambalo Yesu Kristo alilipa Kanisa Lake.
kanisa langu
Kanisa—kundi la watu ambalo wana amini mambo sawa na wana abudu pamoja. Kanisa hili ni la Yesu Kristo. Alilianzisha. Analiongoza. Ni Lake.
litakavyoitwa
Yesu Kristo ametuambia jina lipi Anawataka watu waliite Kanisa Lake. Kwani hivyo ndivyo tunavyopaswa kuliita—na ndivyo kwa upole tunapaswa kuwaomba wengine kuliita vivyo hivyo. Jina hili lilikuja kutoka kwa Yesu Kristo.
siku za mwisho
Siku za mwisho—siku tunazoishi; muda kabla ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Yesu Kristo amelirudisha Kanisa Lake duniani kwa ajili ya wakati huu wa mwisho. Litasaidia kuutayarisha ulimwengu kwa akili ya Ujio Wake wa Pili.
Kanisa la Yesu Kristo
(Ona “kanisa langu.”) Hii ni sehemu ya kwanza ya jina Mwokozi alilolipa Kanisa Lake. Analiita “Kanisa” kwa sababu Yeye alilianzisha. Na Ameliweka jina Lake juu yake.
Siku za mwisho
(Ona “siku za mwisho.”) Hii ni sehemu inayofuata ya jina la Kanisa. Inaonesha kwamba hili ni Kanisa alilolirudisha katika siku hizi, sio lile alilolianzisha hapo mwanzo.
Watakatifu
Watakatifu—neno linalomaanisha “watu walio watakatifu.” Hii ni sehemu ya mwisho ya jina la Kanisa. Inasema kuhusu waumini wa Kanisa. Yesu Kristo anaweza kutufanya safi na halisi. Na anatupa Roho Mtakatifu kutuimarisha tunapojaribu kufanya kile alichotuamuru. Kama tuna imani katika Yeye na kuendelea kujaribu, Yeye hutufanya watakatifu. Hutufanya Watakatifu.
© 2021 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Imepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kiingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, October 2021. Swahili. 17474 743