Kanisa, Jina la
Katika Kitabu cha Mormoni, ni wakati Yesu Kristo alipowatembelea Wanefi wenye haki muda mfupi baada ya Ufufuko Wake, Yeye alisema kwamba Kanisa Lake lapaswa kubeba jina Lake (3 Ne. 27:3–8). Katika nyakati za sasa Bwana alifunulia jina la Kanisa kuwa ni “Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho” (M&M 115:4).