Dhambi Ona pia Chafu, Uchafu; Chukiza, Chukizo; Kosea; Kutokuwa Adilifu, Siyo Adilifu; Ovu, Uovu; Sio mcha mungu; Uasi Kutotii amri za Mungu kwa makusudi. Mtu afichaye dhambi zake hatafanikiwa, Mit. 28:13. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji, Isa. 1:18. Wenye dhambi watakufa, na wenye haki wataokolewa, Eze. 18. Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, Yn. 1:29. Ubatizwe, na ukaoshe dhambi zako, Mdo. 22:16. Mshahara wa dhambi ni mauti, Rum. 6:23. Kwa yeye ajuaye kutenda mema, na wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi, Yak. (Bib.) 4:17. Je, utanifanya kwamba nitetemeke niionapo dhambi, 2 Ne. 4:31. Ole wao wale wafao katika dhambi zao, 2 Ne. 9:38. Hawakuweza kuitazama dhambi isipokuwa kwa chuki, Alma 13:12. Usidhani utarejeshwa kutoka katika dhambi kwenda katika furaha, Alma 41:9–10. Bwana hawezi kuiangalia dhambi na kuivumilia hata kidogo, Alma 45:16 (M&M 1:31). Watoto wadogo hawana uwezo wa kutenda dhambi, Moro. 8:8. Ili kutubu, wanadamu ni lazima waungame na kuacha dhambi zao, M&M 58:42–43. Dhambi kuu zaidi hubaki ndani yake yeye asiye samehe, M&M 64:9. Mtu atendaye dhambi dhidi ya ile nuru kuu zaidi atapata hukumu kuu zaidi, M&M 82:3. Kwa nafsi ile ambayo hutenda dhambi, na dhambi za awali zitamrudia, M&M 82:7. Tunapojaribu kuficha dhambi zetu, mbingu hujitoa zenyewe, M&M 121:37.