Moabu
Nchi katika Agano la Kale iliyokuwa mashariki ya Bahari ya Chumvi. Wamoabu walikuwa ni wazao wa Lutu na walikuwa na uhusiano na Waisraeli. Walizungumza lugha inayofanana na Kiebrania. Kulikuwa na vita vya kudumu baina ya Wamoabu na Waisraeli (Amu. 3:12–30; 11:17; 2 Sam. 8:2; 2 Fal. 3:6–27; 2 Nya. 20:1–25; Isa. 15).