Salemu Ona pia Melkizedeki; Yerusalemu Mji katika Agano la Kale ambao Melkizedeki alitawala. Yawezekana ulikuwa katika eneo ambalo kwa sasa Yerusalemu iko. Jina Salemu linafanana na neno la Kiebrania linalomaanisha “amani.” Melkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, Mwa. 14:18. Melkizedeki, mfalme wa Salemu, alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana, Ebr. 7:1–2. Melkizedeki alikuwa mfalme wa nchi ya Salemu, Alma 13:17–18.