Mtu mwenye haki ya kurithi vipawa vya kimwili au kiroho. Katika maandiko, wenye haki wameahidiwa kwamba watakuwa warithi wa vile vyote Mungu alivyo navyo.
Ibrahimu akawa mrithi wa ulimwengu kwa haki aliyohesabiwa kwa imani, Rum. 4:13 .
Sisi tu watoto wa Mungu, na kama tu watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, na warithi pamoja na Kristo, Rum. 8:16–17 (M&M 84:38 ).
Wewe u mwana, mrithi wa Mungu kwa njia ya Kristo, Gal. 4:7 .
Mungu amemweka Mwanawe kuwa mrithi wa mambo yote, Ebr. 1:2 .
Wale watazamiao msamaha wa dhambi zao ndiyo warithi wa ufalme wa Mungu, Mos. 15:11 .
Watu wakawa watoto wa Kristo na warithi wa ufalme wa Mungu, 4Â Ne. 1:17 .
Watu waliokufa pasipo ufahamu wa injili wataweza kuwa warithi wa ufalme wa selestia, M&M 137:7–8 .
Wafu wanaotubu ni warithi wa wokovu, M&M 138:58–59 .