Makundi maovu ya siri Ona pia Kaini; Wanyangʼanyi wa Gadiantoni Kikundi cha watu walioungana pamoja kwa viapo ili kutekeleza malengo maovu ya kikundi hicho. Baba wa uongo huwachochea watoto wa watu kuwa katika makundi maovu ya siri, 2 Ne. 9:9. Sina budi kuangamiza matendo ya siri ya gizani, 2 Ne. 10:15. Hukumu ya Mungu ilikuja juu ya watendaji hawa wa makundi maovu ya siri, Alma 37:30. Gadiantoni alidhihirisha angamizo lote la watu wa Nefi, Hel. 2:4–13. Shetani aliweka katika mioyo ya watu waunde viapo na maagano ya siri, Hel. 6:21–31. Bwana hafanyi kazi katika makundi maovu ya siri, Eth. 8:19. Mataifa yanayokubali makundi maovu ya siri yataangamizwa, Eth. 8:22–23. Waliyakataa maneno yote ya manabii, kwa sababu ya umoja wao wa siri, Eth. 11:22. Tangu siku za Kaini, palikuwepo makundi ya siri, Musa 5:51.