Moyo Ona pia Moyo Uliovunjika; Zaliwa na Mungu, Zaliwa Tena Ishara ya mawazo na matakwa ya mwanadamu na ishara ya chanzo cha mhemuko wa moyo na hisia zote. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, Kum. 6:5 (Kum. 6:3–7; Mt. 22:37; Lk. 10:27; M&M 59:5). Bwana amemtafuta mtu ampendezaye moyo wake, 1 Sam. 13:14. Mwanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo, 1 Sam. 16:7. Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe atapanda katika mlima wa Bwana naye atabarikiwa, Zab. 24:3–5 (2 Ne. 25:16). Mtu awazavyo katika moyo wake, hivyo ndivyo alivyo, Mit. 23:7. Eliya ataigeuza mioyo ya baba kwa watoto, na mioyo ya watoto kwa baba zao, Mal. 4:5–6 (Lk. 1:17; M&M 2:2; 110:14–15; 138:47; JS—H 1:38–39). Heri wenye moyo safi, Mt. 5:8 (3 Ne. 12:8). Mwanadamu hunena kutoka mema au maovu yaliyo katika moyo wake, Lk. 6:45. Mfuateni Mwana kwa kusudi kamili la moyo, 2 Ne. 31:13. Je, mmezaliwa kiroho kwa Mungu na kuona mabadiliko makubwa katika mioyo yenu, Alma 5:14. Mtoleeni Bwana dhabihu ya moyo uliovunjika na roho iliopondeka, 3 Ne. 9:20 (3 Ne. 12:19; Eth. 4:15; Moro. 6:2). Nitakuambia katika mawazo yako na katika moyo wako kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, M&M 8:2.