Stahimili Ona pia Jaribu, Majaribu; Shida; Subira Kubaki imara katika ahadi na kuwa mkweli katika amri za Mungu licha ya majaribu, upinzani, na shida. Mwenye kustahimili hadi mwisho ataokolewa, Mt. 10:22 (Mk. 13:13). Hawana mizizi na hivyo hustahimili kwa muda mchache, Mk. 4:17. Hisani hustahimili mambo yote, 1Â Kor. 13:7. Baada ya Ibrahimu kustahimili vyema, akapata ahadi, Ebr. 6:15. Kama watavumilia hata mwisho watainuliwa juu katika siku ya mwisho, 1Â Ne. 13:37. Kama mtakuwa watiifu katika amri, na kustahimili hadi mwisho, mtaokolewa, 1Â Ne. 22:31 (Alma 5:13). Kama mtasonga mbele, mkisherehekea karamu ya neno la Kristo, na kustahimili hadi mwisho, mtakuwa na uzima wa milele, 2Â Ne. 31:20 (3Â Ne. 15:9; M&M 14:7). Yeyote ajichukuliae juu yake jina langu, na kustahimili hadi mwisho, ataokolewa, 3Â Ne. 27:6. Yeyote katika Kanisa langu astahimiliye hadi mwisho, huyo nitamstawisha juu ya mwamba wangu, M&M 10:69. Yule astahimiliye katika imani ataushinda ulimwengu, M&M 63:20, 47. Enzi na utawala zote zitakuwa juu ya wote ambao wamestahimili kwa ujasiri mkubwa kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo, M&M 121:29.