Hatia Ona pia Toba, Tubu Hali ya kuwa umetenda baya, au hisia za kujuta na kuhuzunika ambayo huambatana na dhambi. Ametenda dhambi naye anayo hatia, Law. 6:1–6. Yeyote apokeaye sakramenti isivyostahili, atakuwa anajipatia hatia ya mwili na damu ya Yesu, 1 Kor. 11:27. Wenye hatia huichukulia kweli kuwa ngumu, 1 Ne. 16:2. Tutakuwa na ufahamu kamili juu ya hatia zetu zote, 2 Ne. 9:14. Hatia yangu ilifagiliwa mbali, Eno. 1:6. Kulikuwa na adhabu iliyowekwa, ambayo ilileta majuto ya dhamiri, Alma 42:18. Dhambi zako na zikusumbue, usumbufu ambao utakuleta chini kwenye toba, Alma 42:29. Baadhi yenu mna hatia mbele yangu, lakini nitakuwa mwenye rehema, M&M 38:14. Mwana wa Mungu amelipia kosa kwa ajili ya hatia ya mwanzo, Musa 6:54.