Ulimi Ona pia Ndimi, Kipawa cha Ishara ya kunena. Watakatifu wazuie ndimi zao, maana yake ni kwamba wazuie kunena kwao. Ulimi pia una maana ya lugha na watu. Hatimaye, kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kwa Mungu (Isa. 45:23; Rum. 14:11). Uzuie ulimi wako na uovu, Zab. 34:13 (1 Pet. 3:10). Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake atajilinda nafsi yake na taabu, Mit. 21:23. Kama mtu yeyote hauzuii ulimi wake, dini mtu huyo haifai, Yak. (Bib.) 1:26. Kama mtu yeyote hawakosei wengine kwa neno, huyo mtu mkamilifu, Yak. (Bib.) 3:1–13. Injili hii itahubiriwa kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu, Ufu. 14:6–7 (2 Ne. 26:13; Mos. 3:13, 20; M&M 88:103; 112:1). Bwana huyapa mataifa yote, kila taifa na lugha yake, kufundisha neno lake, Alma 29:8. Mabamba yatalifikia kila taifa, kabila, lugha, na watu, Alma 37:4. Lipate neno langu, na ndipo ulimi wako utalegezwa, M&M 11:21. Kila mtu atausikia utimilifu wa injili katika lugha yake mwenyewe, M&M 90:11.