Mavuno Maandiko wakati mwingine hutumia neno mavuno kama ishara ili kumaanisha kuwaleta watu katika Kanisa, ambalo ndilo ufalme wa Mungu duniani, au kwa wakati wa hukumu, kama vile Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, na sisi hatujaokoka, Yer. 8:20 (M&M 56:16). Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache, Mt. 9:37. Mavuno ni mwisho wa ulimwengu, Mt. 13:39. Chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna, Gal. 6:7–9 (M&M 6:33). Shamba ni jeupe tayari kwa mavuno, M&M 4:4. Mavuno yamekwisha na roho zenu hazijaokolewa, M&M 45:2. Wakati wa mavuno umefika, na neno langu lazima litimilike, M&M 101:64.