Onya, Onyo Ona pia Kesha, Walinzi Kutoa taarifa au tahadhari. Manabii, viongozi, na wazazi huonya na kufundisha wengine kuwa watiifu kwa Bwana na mafundisho Yake. Yakobo aliwaonya watu wa Nefi dhidi ya kila aina ya dhambi, Yak. (KM) 3:12. Sauti ya onyo ni kwa watu wote, M&M 1:4. Na kuhubiri kwako kuwe sauti ya onyo, M&M 38:41. Hii ni siku ya kuonya, M&M 63:58. Kila mtu ambaye amekwisha kuonywa yampasa kumwonya jirani yake, M&M 88:81. Nimewaonya na ninawaonya mapema, kwa kuwapa ninyi neno la hekima, M&M 89:4.