Lipa zaka, Zaka Ona pia Fedha; Sadaka, Utoaji sadaka Sehemu moja ya kumi ya mapato ya mtu kwa mwaka aitoayo kwa Bwana kupitia katika Kanisa. Fedha za zaka hutumika kwa kujenga makanisa na mahekalu, kusaidia kazi ya kimisionari, na kujenga ufalme wa Mungu duniani. Ibrahimu alitoa zaka ya vyote alivyokuwa navyo kwa Melkizedeki, Mwa. 14:18–20 (Ebr. 7:1–2, 9; Alma 13:15). Zaka yote ni ya Bwana: ni takatifu kwa Bwana, Law. 27:30–34. Hakika utatoa fungu la kumi la maongezo yako yote, Kum. 14:22, 28. Na zaka za vitu vyote walivileta kwa wingi, 2 Nya. 31:5. Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Tumekuibia katika nini? Katika zaka na matoleo, Mal. 3:8–11 (3 Ne. 24:8–11). Mtu alipaye zaka hataungua moto wakati wa ujio wake, M&M 64:23 (M&M 85:3). Nyumba ya Bwana itajengwa kwa zaka ya watu wake, M&M 97:11–12. Bwana aliifunua sheria ya zaka, M&M 119. Matumizi ya zaka yatapangwa na Baraza, M&M 120.