Ukweli Ona pia Akili, Viumbe-akili-asilia; Maarifa; Nuru, Nuru ya Kristo Ufahamu wa mambo kama yalivyo, na kama yalivyokuwa, na kama yatavyokuwa (M&M 93:24). Ukweli pia unamaanisha nuru na ufunuo kutoka mbinguni. Ukweli utachipua kutoka duniani, Zab. 85:11 (Musa 7:62). Mtaufahamu ukweli, na ukweli utawafanya muwe huru, Yn. 8:32. Mimi ndimi njia, ukweli, na uzima, Yn. 14:6. Kama tutasema hatuna dhambi, ukweli hauko ndani yetu, 1 Yoh. 1:8. Wenye hatia huuchukulia ukweli kuwa ni mgumu, 1 Ne. 16:2. Wenye haki hupenda ukweli, 2 Ne. 9:40. Roho hunena yaliyo ya ukweli na wala hadanganyi, Yak. (KM) 4:13. Wewe u Mungu wa ukweli na huwezi kudanganya, Eth. 3:12. Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu waweza kujua ukweli wa mambo yote, Moro. 10:5. Ukweli hudumu milele na milele, M&M 1:39. Wewe umeangaziwa na Roho wa ukweli, M&M 6:15. Kitabu cha Mormoni kina ukweli na neno la Mungu, M&M 19:26. Mfariji alipelekwa kufundisha ukweli, M&M 50:14. Mtu ambaye hulipokea neno kwa Roho wa ukweli huupokea kama linavyohubiriwa na Roho wa ukweli, M&M 50:17–22. Tangazeni ukweli kulingana na mafunuo niliyowapeni, M&M 75:3–4. Lolote lililo la kweli ni nuru, M&M 84:45. Nuru ya Kristo ni nuru ya ukweli, M&M 88:6–7, 40. Roho yangu ni ukweli, M&M 88:66. Akili, au nuru ya kweli, haikuumbwa, M&M 93:29. Utukufu wa Mungu ni akili, au nuru na ukweli, M&M 93:36. Nimewaamuru ninyi kuwalea watoto wenu katika nuru na ukweli, M&M 93:40. Mwanangu wa Pekee amejaa neema na ukweli, Musa 1:6.