Wayaredi
Watu katika Kitabu cha Mormoni ambao walikuwa wazao wa Yaredi, kaka yake, na marafiki zao (Eth. 1:33–41). Waliongozwa na Mungu kutoka Mnara wa Babeli hadi Marekani, nchi ya ahadi (Eth. 1:42–43; 2–3; 6:1–18). Ingawa taifa lao wakati fulani lilikuwa na mamilioni ya watu, wote walijiangamiza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoletwa na uovu (Eth. 14–15).