Dani
Katika Agano la Kale, huyu ni mwana wa Yakobo na Bilha, mjakazi wa Raheli (Mwa. 30:5–6).
Kabila la Dani
Kwa baraka za Yakobo juu ya Dani, ona Mwanzo 49:16–18. Kwa baraka za Musa juu ya kabila la Dani, ona Kumbukumbu la Torati 33:22. Baada ya kukaa katika Kanaani, kabila la Dani lilipata kipande kidogo cha ardhi lakini chenye rutuba (Yos. 19:40–48). Walikuwa na kazi ngumu ya kuulinda dhidi ya Waamori (Amu. 1:34) na dhidi ya Wafilisti (Amu. 13:2, 25; 18:1). Kama matokeo yake, Wadani walihamia kaskazini ya Palestina (Amu. 18), karibu ya Laishi, na wakauita mji ule Dani. Mji huu unajulikana vizuri kama mpaka wa kaskazini wa Palestina, ambao ulienea “kutoka Dani hadi Beer-sheba.”