Kuwakubali Viongozi wa Kanisa Ona pia Ridhaa ya Wengi Kutoa ahadi ya kuwaunga mkono viongozi wakuu wa Kanisa au wa maeneo yetu walio katika nafasi za uongozi. Ukamweke Yoshua mbele ya mkutano wote, na ukampe mausia mbele ya macho yao, Hes. 27:18–19. Watu wote wakapiga kelele, na kusema, Mungu mwokoe mfalme, 1 Sam. 10:24. Waamini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa, 2 Nya. 20:20. Watiini wao walio watawala juu yenu, Ebr. 13:17. Wewe utapendelewa na Bwana, kwa sababu wewe hujanungʼunika, 1 Ne. 3:6. Waliowapokea manabii walihurumiwa, 3 Ne. 10:12–13. Sikilizeni maneno ya hawa Kumi na wawili, 3 Ne. 12:1. Kwa sauti yangu mimi mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa, M&M 1:38. Maneno yake mtayapokea, kama vile yatoka kinywani mwangu mwenyewe, M&M 21:5. Yeye awapokeaye watumishi wangu, hunipokea mimi, M&M 84:35–38. Yeyote anipokeaye mimi, huwapokea wale niliowatuma, M&M 112:20. Kama watu wangu hawatasikiliza sauti za watu hawa ambao nimewateua, hawatabarikiwa, M&M 124:45–46.