Mauaji Ona pia Adhabu Kuu; Kaini Kwa makusudi na pasipo uhali mtu anatwaa uhai wa mtu mwingine. Mauaji ni dhambi iliyolaaniwa tangu nyakati za mwanzo (Mwa. 4:1–12; Musa 5:18–41). Yeyote atakaye mwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, Mwa. 9:6 (TJS, Mwa. 9:12–13; Ku. 21:12; Alma 34:12). Usiue, Ku. 20:13 (Kum. 5:17; Mt. 5:21–22; Mos. 13:21; M&M 59:6). Yesu alisema, usiue, Mt. 19:18. Wauaji watakuwa na sehemu yao katika mauti ya pili, Ufu. 21:8. Ninyi ni wauaji mioyoni mwenu, 1 Ne. 17:44. Ole kwa muuaji anayeua kwa kutaka, 2 Ne. 9:35. Mungu ameamuru kwamba wanadamu wasiue, 2 Ne. 26:32. Mauaji ni chukizo kwa Bwana, Alma 39:5–6. Yule anayeua hatapata msamaha, M&M 42:18. Mtu yeyote atakayeua atolewe na kushughulikiwa kulingana na sheria za nchi, M&M 42:79.