Haruni, Kaka wa Musa Ona pia Musa; Ukuhani wa Haruni Katika Agano la Kale, ni mwana wa Amramu na Yokebedi, wa kabila la Lawi (Ku. 6:16–20); kaka mkubwa wa Musa (Ku. 7:7). Aliteuliwa na Bwana ili kumsaidia Musa katika kuwaleta wana wa Israeli kutoka Misri na kuwa msemaji wake, Ku. 4:10–16, 27–31; 5:1–12:51. Juu ya Mlima Sinai, Musa alipokea maelekezo juu ya uteuzi wa Haruni na wanawe wanne kwenye Ukuhani wa Haruni, Ku. 28:1–4. Kwa maombi ya watu alitengeneza ndama wa dhahabu, Ku. 32:1–6, 21, 24, 35. Alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123, Hes. 20:22–29 (Hes. 33:38–39). Bwana alithibitisha ukuhani pia juu ya Haruni na uzao wake, M&M 84:18, 26–27, 30. Wale wenye kukuza miito ya ukuhani huwa wana wa Musa na Haruni, M&M 84:33–34.