Misaada ya Kujifunza
Mwonaji


Mwonaji

Mtu aliyeruhusiwa na Mungu kuona kwa macho ya kiroho mambo yale ambayo Mungu ameyaficha kwa ulimwengu (Musa 6:35–38). Yeye ni mfunuzi na nabii (Mos. 8:13–16). Katika Kitabu cha Mormoni, Amoni alifundisha kwamba mwonaji pekee aliweza kutumia vitafsiri maalumu, au Urimu na Thumimu (Mos. 8:13; 28:16). Mwonaji hujua yaliyopita, yaliyopo, na yajayo. Zamani, nabii mara kwa mara aliitwa mwonaji (1 Sam. 9:9; 2 Sam. 24:11).

Joseph Smith ndiye mwonaji mkuu wa siku za mwisho (M&M 21:1; 135:3). Kwa nyongeza, Urais wa Kwanza na Baraza la wale Kumi na Wawili wanakubalika kama manabii, waonaji, na wafunuzi.