Smith, Joseph, Mkubwa Ona pia Smith, Joseph, Mdogo; Smith, Lucy Mack Baba wa Joseph Smith Nabii. Alizaliwa 12 Julai 1771. Alimwoa Lucy Mack, na walizaa watoto tisa (JS—H 1:4). Joseph alikuwa muumini mwaminifu katika Urejesho wa siku za mwisho na Patriaki wa kwanza kwa Kanisa. Alikufa 14 Septemba 1840. Mungu alimfunulia maelekezo kupitia mwanawe Joseph, M&M 4; 23:5. Mwacheni mtumishi wangu mzee aendelee kukaa pamoja na familia yake, M&M 90:20. Mtumishi wangu mzee Joseph hukaa pamoja na Ibrahimu katika mkono wake wa kuume, M&M 124:19. Joseph Smith Mdogo, alimwona baba yake katika ono la ufalme wa selestia, M&M 137:5. Malaika alimwamuru Joseph Smith Mdogo umwambia baba yake juu ya ono alilopata, JS—H 1:49–50.