Helamani, Wana wa Ona pia Helamani, Mwana wa Alma; Waanti-Nefi-Lehi Katika Kitabu cha Mormoni, ni wana wa Walamani walioongolewa waliojulikana kama Waamoni ambao walikuwa askari wa vita chini ya uongozi wa Helamani (Alma 53:16–22). Helamani aliwaona kuwa wanastahili kuitwa wanawe, Alma 56:10. Mama zao walikuwa wamewafundisha kutokuwa na mashaka na uwezo wa Bwana wa kuwakomboa, Alma 56:47. Waliwashinda Walamani na walilindwa na imani yao kiasi kwamba hakuna yeyote aliyeuawa, Alma 56:52–54, 56; 57:26.