Shutuma, Shutumu Ona pia Amua, Hukumu; Hukumu ya mwisho Kuamua au kutiwa hatiani na Mungu. Mungu atamhukumu mtu mwenye hila, Mit. 12:2. Twarudiwa na Bwana, ili tusipaswe kuhukumiwa pamoja na ulimwengu, 1 Kor. 11:32. Maneno yetu, matendo, na mawazo yetu yatatuhukumu, Alma 12:14. Kwa kujua mambo na kuacha kuyatenda, watu huwa chini ya hukumu, Hel. 14:19. Kama tutakoma kufanya kazi, itatupasa kuwekwa chini ya hukumu, Moro. 9:6. Mtu asiye msamehe ndugu yake husimama akiwa na hatia mbele ya Bwana, M&M 64:9. Yule atendaye dhambi dhidi ya nuru kubwa zaidi atapokea hukumu kubwa zaidi, M&M 82:3. Kanisa lote liko chini ya hatia hadi watakapotubu na kukumbuka Kitabu cha Mormoni, M&M 84:54–57.