Kanaani, Mkananayo
Katika nyakati za Agano la Kale, ni mtoto wa nne wa kiume wa Hamu (Mwa. 9:22; 10:1, 6) na ni mjukuu wa Nuhu. Mkananayo humwelezea mtu aliyetoka nchi ambako Kanaani mwanzoni aliishi na pia kwa wazao wake. Mkananayo lilikuwa pia jina la watu ambao waliishi nchi za bondeni kando ya pwani ya Mediterania ya Palestina. Jina hili wakati mwingine lilitumika kuwaelezea watu wasio Waisraeli walio wakazi wa nchi ya magharibi mwa Yordani, ambao Wayunani waliwaita Wafoeniki.