Misaada ya Kujifunza
Wasamaria


Wasamaria

Watu wa nyakati za Biblia walioishi katika Samaria baada ya ufalme wa kaskazini wa Israeli kutekwa na Waashuru. Wasamaria walikuwa sehemu ni Waisraeli na sehemu ni Wayunani. Dini yao ilikuwa ni mchanganyiko wa imani na desturi za Kiyahudi na kipagani. Mfano wa Msamaria mwema katika Luka 10:25–37 unaonyesha chuki ambayo Wayahudi waliikuza kwa Wasamaria kwa sababu Wasamaria walikuwa wamekengeuka kutoka dini ya Kiisraeli. Bwana aliwatuma Mitume kufundisha injili kwa Wasamaria (Mdo. 1:6–8). Filipo kwa mafanikio alihubiri injili ya Kristo kwa watu wa Samaria na akafanya miujiza mingi miongoni mwao (Mdo. 8:5–39).