Tarajio la hamu ya uhakika la baraka za haki zilizoahidiwa. Maandiko mara kwa mara huzungumza juu ya tumaini kama matarajio ya uzima wa milele kupitia imani katika Yesu Kristo.
Heri mtu yule ambaye tumaini lake ni Bwana, Yer. 17:7 .
Bwana atakuwa ndiye tumaini la watu wake, Yoe. 3:16 .
Tunalo tumaini kwa njia ya subira na maandiko, Rum. 15:4 .
Mungu ametuzaa sisi kwa tumaini lenye uzima katika ufufuko wa Kristo, 1Â Pet. 1:3 .
Kila mwanadamu aliye na tumaini hili hujitakasa yeye mwenyewe, 1 Yoh. 3:2–3 .
Lazima msonge mbele, mkiwa na mwangaza kamili wa tumaini, 2Â Ne. 31:20 .
Angalieni kuwa mnayo imani, tumaini, na hisani, Alma 7:24 (1Â Kor. 13:13 ; Moro. 10:20 ).
Ningelitamani muyasikie maneno yangu, mkiwa na tumaini ya kwamba mtapokea uzima wa milele, Alma 13:27–29 .
Kama mna imani, ninyi mnalo tumaini kwa ajili ya mambo yasiyoonekana, ambayo ni ya kweli, Alma 32:21 (Ebr. 11:1 ).
Tumaini huja kwa imani ambayo hufanya nanga kwa roho, Eth. 12:4 (Ebr. 6:17–19 ).
Mwanadamu lazima awe na tumaini vinginevyo hataweza kupokea urithi, Eth. 12:32 .
Mormoni alizungumza juu ya imani, tumaini, na hisani, Moro. 7:1 .
Mtakuwa na tumaini kupitia upatanishi wa Yesu Kristo la kufufuliwa katika uzima wa milele, Moro. 7:40–43 .
Roho Mtakatifu hukujaza matumaini, Moro. 8:26 (Rum. 15:13 ).