Ufungwa Ona pia Huru, Uhuru Kuwa katika hali ya utumwa wa kimwili au kiroho. Nyumba ya Israeli ilienda kifungoni kwa sababu ya uovu wao, Eze. 39:23. Yule aongozaye kifungoni atakwenda kifungoni, Ufu. 13:10. Waovu watatupwa chini katika utumwa wa ibilisi, 1 Ne. 14:4, 7. Wanadamu wako huru kuchagua uhuru na uzima wa milele au utumwa na mauti, 2 Ne. 2:27. Mapenzi ya mwili hutoa uwezo kwa roho wa ibilisi kuteka nyara, 2 Ne. 2:29. Je, mngali mnakumbuka vya kutosha utumwa wa mababu zenu, Alma 5:5–6. Wale wenye kushupaza mioyo yao huchukuliwa mateka na ibilisi, Alma 12:11. Kesheni na kusali daima, msije mkajaribiwa na ibilisi, nanyi mkaongozwa utumwani na yeye, 3 Ne. 18:15.